LIVE STREAM ADS

Header Ads

JAMANI TAZAMENI AIRTEL RISING STAR IKIZINDULIWA MKOANI MWANZA. NI KWELI TANZANIA BILA SOKA INAWEZEKANA?

Mashindano ya Airtel Rising Star ambayo yanayoshiriki wachezaji walio na Umri chini ya Miaka 17 jana yameanza Rasmi Mkoani Mwanza ambapo
Timu ya Alliance Sports Academy ilikuwa ikimenyana na Timu ya TSC Sport Academy katika Uwanja wa CCM Kirumba. Katika Mechi ya Ufunguzi Timu ya Alliance Academy iliichakaza Timu ya TSC Academy kwa bao 4-2.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslauns Mabula ambae alikuwa Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mashindano ya Airtel Rising Star yanayoshirikisha Watoto walio na Umri chini ya Miaka 17 hapa nchini. Hapa alikuwa akizungumza katika Ufunguzi wa Mashindano hayo Mkoani Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba. Mabula alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza (MZFA) Nasib Maburuki akizungumza katika Ufunguzi wa Michuano ya Airtel Rising Star iliyofunguliwa Rasmi jana katika Uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza.
Raphael Daudi ambae ni Meneja Masoko wa Airtel Kanda ya Ziwa akizungumza katika Ufunguzi wa Michuano ya Airtel Rising Star iliyofunguliwa Rasmi jana katika Uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza.
Kikosi cha TSC Academiy kinachoshiriki Mashindano ya Airtel Rising Star Mkoani Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslauns Mabula (Mwenye nguo nyeusi) akikagua kikosi cha Timu ya TSC Academy Kinachoshiriki Michuano ya Airtel Rising Star Mkoani Mwanza.
Kikosi cha Alliance Academy Kinachoshiriki Mashindano ya Airtel Rising Star Mkoani Mwanza.
Kikosi cha Alliance Academy Kinachoshiriki Mashindano ya Airtel Rising Star Mkoani Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslauns Mabula (Mwenye nguo nyeusi) akikagua kikosi cha Timu ya Alliance Sports Academy Kinachoshiriki Michuano ya Airtel Rising Star Mkoani Mwanza.
Kikosi cha Alliance Academy Kinachoshiriki Mashindano ya Airtel Rising Star Mkoani Mwanza.
Kikosi cha Alliance Academy Kinachoshiriki Mashindano ya Airtel Rising Star Mkoani Mwanza.
Kikosi cha TSC Academiy kinachoshiriki Mashindano ya Airtel Rising Star Mkoani Mwanza.
Waamuzi wa Mashindano ya Airtel Rising Star katika Mechi ya Ufunguzi baina ya Alliance Sports Academy na TSC Academy.
Makeputeni na Waamuzi wa Mashindano ya Airtel Rising Star katika Mechi ya Ufunguzi baina ya Alliance Sports Academy na TSC Academy.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza na Diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslauns Mabula akipiga Mpira golini kama ishara ya Ufunguzi wa Mashindano ya Airtel Rising Star Mkoani Mwanza .Mashindano haya yamefunguliwa katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.