LIVE STREAM ADS

Header Ads

OXS OKELEKY FT. MO MUSIC & NATTY E NDANI YA BASI NENDA RMX. ISIKILIZE NA KUIDOWNLOAN HAPA.

Basi Nenda ambayo ni ngoma ya Kwake Msanii Mo-Music kutoka Jijini Mwanza imeendelea kufanya vyema katika anga ya musiki hapa nchini huku msanii huyo akiwa
tayari ameanza kuonja matunda ya kazi yake.

Mo-Music tayari ameanza kushirikishwa na wasanii wengine wakubwa hapa nchini ambapo tayari Kala Jeremiah amemshirikisha Mo katika ngoma aliyomshirikisha pia Ney wa Mitego ambayo inafahamika kama Simu ya Mwisho.

Ili kuwapa radha nyingine, Msanii Ox Okeleky ameamua kuurudia wimbo wa Basi Nenda ambapo humo ndani amemshirikisha Mwana dada Natty E pamoja na Mo Music mwenyewe wote wakiwa wanatoka Jijini Mwanza. Mbali na Music Natty ni Mtangazaji na Oxs ni Producer wa Vipindi vya Radio na Music wote wakiwa wanafanya kazi na Radio Metro ya Jijini Mwanza.

ISIKILIZE HAPA BASI NENDA RMX AKIWA AMEIRUDIA KATIKA STUDIO ILE ILE YA K.RECORDS CHINI YA PRODUCER LOL POP.


Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.