MSHINDI MISS LAKE ZONE 2014 HUYU HAPA. AONDOKA NA GARI LENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 10.

Mshindi wa Miss Lake Zone 2014
Rachael Clavery (katikati) akila pozi katika picha ya ukumbusho na mshindi wa pili Mary Emanuel( kulia) na Mshindi wa tatu Nikole Sarakikya (kushoto). Rachael amejinyakulia zawadi nono ya Gari la millioni 10 katika Shindano la Miss Lake Zone 2014 lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza.

Warembo waliopanda Jukwaani na Mikoa yao kwenye mabano ni Moshy Shaban; Doreen
Robert; Christina Jilulu (Mwanza); Nikole Sarakikya, Mary Emanuel na
Rachael Julika (Shinyanga).
Wengine ni Faudhia Haruna, Jackline Kimambo na Christina John (Kagera), huku Nyangi Warioba; Cecilia Kibada na Everlyn Charles (Simiyu), Martina John; Elinaja Nnko, Winfrida Nashon (Mara) huku Rose Msuya, Rachael Clavery na Faridha Ramadhani wakiwakilisha mkoa wa Geita. Hadi hapo tayari umejua Taji la Miss Lake Zone 2014 limeenda Mkoani Geita.

Kwenye picha ya pamoja

Awali
akizungumzia Shindano hilo Mkurugenzi wa Kampuni ya Flora Promotion iliyoandaa
Shindano la Miss Lake Zone 2014, Flora Lauwo zawadi ya gari iliyotolewa na
mmoja wa wadhamini wa shindano hilo, Lenny Hotel chini ya Mkurugenzi wake
Leonard imeongeza chachu ya ushindani katika Shindano hilo.
Flora ambaye ni mara ya tatu kuandaa shindano hilo la Kanda ya Ziwa, amewahi kutoa mara mbili mshindi wa Miss Tanzania (2008 na 2009), Nasrim Karim na Miriam Gerrard ambapo kwa upande wa kiingilio ilikuwa bei chee kabisa kwani viti maalum ilikuwa shilingi 30,000; viti vya jukwaa kuu ni sh 10,000 na viti vya kawaida ni sh 5,000.

Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.
No comments: