LIVE STREAM ADS

Header Ads

PROFESA MAHALU ACHANGISHA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 38 SHULE YA GREEN VIEW. NI KATIKA KUADHIMISHA JUBILEE YA MIAKA 25 YA SHULE HIYO.

Katika kuadhimisha Jubilee ya Miaka 25 tangu kuanzishwa Shule ya Green View iliyoko Mkoani Mwanza, Zaidi ya Shilingi Milioni 38 zimeweza kupatikana katika harambee kwa ajili ya Ujenzi wa Bweni la Wasichana wa Shule hiyo.

Sherehe za Maadhimisho ya Jubilee hiyo zilifanyika
jana Kiseke Wilayani Ilemela ziliko shule za Sekondari na Msingi Green View, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Rufaa Bugando Profesa Dr.William Mahalu.
Katika Sherehe hizo ambazo zilihudhuliwa na wageni mbalimbali, Profesa Dr.Mahalu aliongoza Harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Green View.

Katika Harambee hiyo ambayo iliwahusisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wazazi, jumla ya Shilingi 38, 514,500 ziliweza kupatikana huku takribani Shilingi Milioni 36 zikipatina papo hapo ambapo ahadi ilikuwa takribani shilingi Milioni 2 huku Vigae boksi tano pamoja na Mifuko ya Theluji 102 ikitolewa katika Harambee hiyo.
Asia Kapande ambae ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule za Green View (Kulia) Akimlisha Keki Mgeni Rasmi Kaimu Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Rufaa Bugando Profesa Dr.William Mahalu. 

Kwa Mara ya Kwanza Shule ya Green View ilianzishwa mwaka 1989 ikiwa na darasa la Awali pekee ambapo iliendelea kukua hadi kufikia hivi sasa ambapo kuna Shule ya Awali, Shule ya Msingi na Sule ya Sekondari huku Matarajio ya uongozi wa Shule hizo yakiwa ni kupanuka zaidi na kuwa na Kidato cha Tano na Sita sanjari na Kuanzisha pia Chuo.

Akizungumza katika Sherehe za Jubilee hiyo ya kutimiza Miaka 25 ya Green View, Bonny Matemba ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shule za Green View alibainisha kuwa Shule za Green View zimelenga katika Kumpatia mwanafunzi elimu bora ambayo itamuwezesha kupambana na changamoto za maisha na hatimae kufikia katika mafanikio yake.
Asia Kapande ambae ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule za Green View (Kulia) Akilishwa Keki Mgeni Rasmi Kaimu Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Rufaa Bugando Profesa Dr.William Mahalu (Kushoto). 

Aidha aliongeza kuwa, awali kabla ya Kuanzishwa kwa shule za Green View wazazi wengi walikuwa na hurka ya kuwapeleka watoto wao kusoma nje ya nchi, jambo ambalo kwa sasa halipo tena baada ya Shule za Green View kuanzishwa kutokana na elimu bora inayotolewa na Shule hizo ambazo zinatumia mitaala ya kiingereza kufundishia.

Akizungumzia mafanikio ya Shule za Green View, Matemba alibainisha kwamba kwa miaka takribani yote, wanafunzi wake wamekuwa wakifaulu katika mitihani yao huku akiitolea mfano mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne na darasa la saba ya mwaka jana kwamba wanafunzi wote wa shule za Green View waliweza kufaulu mitihani yao.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Rufaa Bugando Profesa Dr.William Mahalu (Kushoto) akimlisha Keki Mkurugenzi Mtendaji wa Shule za Green View Bonny Matemba (Kushoto).

Nao baadhi ya Wanafunzi waliowahi kusoma katika Shule za Green View ambao walifika katika Jubilee hiyo ya Miaka 25 tangu kuanzishwa kwake walielezea furaha yao kwamba, elimu bora waliyoipata imewajengea msingi imara katika kufikia mafanikio yao ya kielimu na kimaisha pia.

Kaka Mkuu nae akalishwa Keki na Mgeni Rasmi.
Ikafuata zamu ya Dada Mkuu nae kulishwa Keki na Mgeni Rasmi.
Shampeini nazo kama kawa zilikuwepo.
"Waooooooooh"
Wageni Waalikwa.
Viongozi wa Bodi wa Shule za Green View wakiwa na Mgeni Rasmi Meza Kuu.
Viongozi wa Bodi wa Shule za Green View.
Viongozi wa Bodi wa Shule za Green View.
Wazazi wakiwa makini kufuatilia burudani zilizokuwa zikitolewa katika Sherehe ya Kuadhimisha Jubilee ya Miaka 25 tangu kuanzishwa Shule ya Green View mwaka 1989.
Wazazi waliofika katika Sherehe hiyo.
Wanafunzi wakitoa Burudani.
Wanafunzi wa Green View wakitoa burudani.
Ngoma ya Bujora ikitokea Burudani katika Sherehe hizo za Jubilee ya Miaka 25 tangu kuanzishwa Shule ya Green View.
"Kitu iliingizwa mdomoni. Chezea Bujora"
"Dogo alitetemeka mwili mzima"
Rasta Boy akiwa na baadhi ya Wanafunzi wenzake wa Green View Scool.
Rasta Girl akifurahi na Mtanzania Media. Huyu ni Mdogo wake na Rasta Boy uliemuona picha ya juu.
Mgeni Mwalikwa kutoka Kampuni ya Ulinzi ya KK-Security akitoka kuwatuza wachezaji wa ngoma za asili kutoka Bujora.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.