|
Kikundi cha Ngoma Asilia kutoka Bujora Mkoani Mwanza kikitumbuiza katika Ufunguzi huo. Na huu ni mchezo wa Kucheza na Nyoka. Read More kujionea kilichojili.
|
Vijana na Jamii nzima kwa ujumla
wameshauriwa kuzingatia mfumo wa njia za Uzazi wa Mpango katika kupanga
familia, kwa kuwa mfumo huo utawawezesha wanafalia kupanga familia watakayoweza
kuihudumia sanjari na vijana kufikia malengo yao.
Ushauri huo
ulitolewa hii jana Mkoani Mwanza na Elly Rewete ambae ni Mkurugenzi wa Rasilimali
watu na Utawala kutoka Marie Stopes Tanzania, katika Uzinduzi wa Kitua cha Afya
cha Marie Stopes kilichopo Nyegezi Wilayani Nyamagana.
Rewete ambae
alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Marie Stopes katika Uzinduzi huo, alibainisha
kuwa Uzazi wa Mpango ndiyo njia pekee inayoweza kuondoa vikwazo vya Mimba
zisizotarajiwa, Kufikia Malengo kielimu pamoja na kupambana na umasikini na
hatimae kuchangia katika pato la Taifa.
|
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Valentino Francis Bangi akiwa tayari kabisa kwa ajili ya kukata Utepe kama ishara ya ufunguzi wa Kituo hicho cha Afya cha Marie Stopes Nyegezi. |
|
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Valentino Francis Bangi akikata Utepe kama ishara ya ufunguzi wa Kituo hicho cha Afya cha Marie Stopes Nyegezi Jijini Mwanza. |
Akizungumza
kwa niaba ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mganga Mkuu wa Mkoa Mwanza
Valentino Francis Bangi alitoa rai kwa wanafamilia wote kushiriki katika njia
za Uzazi wa Mpango badala ya suala hilo kuachiwa wanawake pekee.
Aidha
alisisitiza kwamba makundi yote yanayostahili kupata huduma za Afya bure katika
jamii, yanapaswa kutambuliwa ambapo zaidi amesisitiza kundi la wazee walio na
umri wa miaka 60 na kuendelea kuandikishwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu bila
malipo kupitia huduma ya tiba kwa kadi.
Baada ya
agizo hilo, Diwani wa Kata ya Butimba Masunu Dismas Masunu akabainisha kwamba
Kata ya Butimba na Jiji la Mwanza kwa ujumla imekwisha anza utekelezaji wa
kuhakikisha kwamba wazee wote wanatibiwa bure, ambapo jumla ya wazee 902 wamekwisha
pewa vitambulisha vya matibabu ya bure ambapo katika Kata ya Butimba Wazee
takribani 113 tayari wamepewa vitambulisho hivyo.
Nao baadhi
ya wananchi hususani vijana waliofika katika uzinduzi wa kituo hicho cha Marie
Stope kilichopo Nyegezi Wilayani Nyamagana, walieleeza kwamba suala la Uzazi wa
Mpango bado halijaeleweka sana katika jamii hivyo ni vyema elimu zaidi ikazidi
kutolewa kwa vijana na wananchi wote kwa ujumla ili kuwaongezea uelewa zaidi
kuhusiana na masuala ya uzazi wa mpango.
|
Elly Rewete ambae ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na
Utawala kutoka Marie Stopes Tanzania (Kushoto), akifuatiwa na Miss Tanzania Happness Watimanywa (Katikati) na wa mwisho (kulia) ni Miss
Marie Stopes Narietha Boniphace.
|
|
Miss Tanzania Happness Watimanywa (Kushoto) akiwa na Miss
Marie Stopes Narietha Boniphace (Kulia). Wote ni Mabalozi wa Marie
Stopes ambao wanahamasisha vijana na wanajamii kwa ujumla kuzingatia
njia za uzazi wa mpango. |
|
Wananchi waliofika katika uzinduzi huo. |
|
Kuanzia Agost 25 hadi jana Agost 29 Huduma mbalimbali za Uzazi wa Mpango zilitolewa bure kwa wananchi kama sehemu ya Ufunguzi wa Kituo hicho. Huduma zilizotolewa ni pamoja na Kufunga Uzazi kwa akina mama, akina baba, kuweka kitanzi, kipandikizi na sanjari na huduma nyinginezo zote za uzazi mpango. |
|
Miss Tanzania Happness Watimanywa. |
|
Miss Tanzania Happness Watimanywa |
|
Elly Rewete ambae ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na
Utawala kutoka Marie Stopes Tanzania. |
|
Diwani wa Kata ya Butimba Jijini Mwanza Masunu Dismas Masunu. |
|
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Valentino Francis Bangi. |
|
Mwanahabari kutoka Kwa Neema Radio Joel Maduka (Katikati) akiwa na Miss Tanzania Happness Watimanywa (Kushoto) pamoja na Miss Marie Stopes Narietha Boniphace (Kulia). |
|
Mkurugenzi wa Mtanzania Media na Mwanahabari kutoka Radio Metro George Binagi (Katikati) akiwa na Miss Tanzania Happness Watimanywa (Kushoto) pamoja na Miss Marie Stopes Narietha Boniphace (Kulia). |
|
Miss Tanzania Happness Watimanywa (Kushoto) akiwa na Miss Marie Stopes Narietha Boniphace (Kulia). Wote ni Mabalozi wa Marie Stopes ambao wanahamasisha vijana na wanajamii kwa ujumla kuzingatia njia za uzazi wa mpango. |
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.
No comments: