Zawadi za Washindi wa Shindano laMiss Lake Zone 2014 linalotarajiwa kufanyika hii leo jumamosi Agost 30
katika Uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza tayari zimewekwa hadharani.
Flora Lauwo
ambae ni muandaaji wa Shindano hilo kupitia kampuni yake ya Flora Promotion
amebainisha kuwa,
Mshindi wa Kwanza atapata zawadi ya gari yenye thamani ya
shilingi Milioni Kumi, Mshindi wa Pili atajipatia zawadi Bajaji yenye tahamani
ya shilingi milioni nne, ambapo mshindi wa tatu atapata fursa ya kusomeshwa
huku mrembo mwenye kipaji akijishindia zawadi ya pikipiki yenye thamani ya
shilingi Milioni moja na laki sita sanjari na zawadi mbalimbali kutoka kwa wadhamni.
Kwa upande
wake Benny Mwangi ambae ni Meneja wa Lenny Hotel iliyopo Mkoani Geita, ameeleza
kuwa Lenny Hotel ilijitokeza kudhamini shindano hilo kwa lengo la kuboresha
mashindano hayo, huku akiongeza kuwa jamii inapaswa kubadili mtizamo na kuachana
na fikra potofu kuwa mashindano ya urembo ni uhuni. Lenny Hotel katika udhamini
wake imetoa zawadi ya gari yenye thamani ya shilingi Milioni kumi kwa ajili ya
mshindi wa kwanza.
Nao Washiriki
wa Shindano hilo wameelezea furaha yao baada ya kuchaguliwa kuiwakilisha Mikoa
yao ya Kanda ya Ziwa, ambapo kila Mkoa umetoa Washiriki watatu kwa ajili ya
kujishiriki Shindano hilo la Miss Lake Zone 2014 ambapo kiingilio kimepangwa
kuwa ni shilingi 5,000, 10,000 na 30,000.
Kila Mmoja
wa washiriki hao amejigamba kuibuka mshindi wa kwanza na hivyo kuondoka na zawadi ya gari ambapo wamewasihi wakazi
wa Kanda ya Ziwa ikiwemo Mkoa wa Mwanza kujitokeze kwa wingi hii leo katika Uwanja wa CCMK Kirumba ili kushuhudia shindano hilo la Miss Lake Zone 2014.
 |
"Mtoto Mtoto" |
 |
Funguo za Gari kwa ajili ya Mshindi wa Kwanza wa Miss Lake Zone 2014. |
 |
Judith Josephat Maturege (Kulia) ambae ni Matron wa Mamiss wanaoshiriki shindano hilo akishow love na mdau. |
 |
"Matron bwana alitokea kuvutiwa na Pen yangu...ikabidi nimuachie" |
 |
Benny Mwangi ambae ni Meneja wa Lenny Hotel iliyopo
Mkoani Geita. |
 |
Benny Mwangi ambae ni Meneja wa Lenny Hotel iliyopo
Mkoani Geita akiwa katika mahojiano na Wanahabari. |
 |
Wadau wakichukua kumbukumbu. |
 |
Zawadi za Washindi wa Miss Lake Zone 2014. |
 |
Watoto wanapendeza kiukweli. Hutakiwi kukosa leo katika Uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza. Jukwaani atakuwepo Barnaba Boy pamoja na SkyLite Band. |
Na: George Binago @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.
No comments: