LIVE STREAM ADS

Header Ads

NI MWENDO WA NGOMA MBILI MBILI. MR. B NAE AACHIA NYOMA MBILI KWA WAKATI MMOJA.

Mr. B
Msaani Chipukizi Kutoka Jijini Mwanza ambae anafahamika kwa jina la Mr. B ameachia ngoma zake mbili kwa wakati mmoja ambapo yeye anasema
anaamini kuwa kuachia ngoma mbili kwa wakati mmoja itakuwa ni fursa nzuri kwa Mashabiki wa Mziki wa Bongo kuweza kutambua haratakazti zake.

Mr. B amesema kwamba kikubwa kilichosababisha hadi akaachia ngoma hizo kwa wakati mmoja ni kuweza kuwapa burudani wapenzi wa Mziki hapa nchini kwa kuwa kila wimbo una mashairi na Mahadhi tofauti hivyo hiyo itakuwa ni fursa kwake kuwakamata mashabiki zake wote.

Ngoma ya Kwanza inafahamika kama Kaa Chonjo ambayo amefanya na Monkara 111 katika Studio za Kweya Records chini ya Producer Bravo ambapo humo ndani amezungumzia zaidi Harakati za kutafuta Life, huku ngoma ya Pili akiwa amesimama peke yake na inafahamika kama Baby ambapo katika ngoma hiyo zaidi amezungumzia Mapenzi.

ISIKILIZE YA NGOMA YA KAA "CHONJO" HAPA.


Mr. B>>>Mawasiliano 0769 48 7137.
Mr. B anakuwa ni Msaani wa Pili kwa siku za hizi karibuni kuachia ngoma mbili kwa wakati mmoja huku akiwa ni msanii wa kwanza kwa wasanii wanaochipukia, baada ya Mkali wa Bongo Fleva Ali Kiba kuachia ngoma zake mbili kwa wakati mmoja ya kwanza ikiwa ni Kimasomaso na ya pili ikiwa ni Mwanza Dar es salaam ambapo zote kwa pamoja zimepokelewa vyema na wapenda burudani hapa nchini.
ISIKILIZE NGOMA YA "BBABY" HAPA.

Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.