LIVE STREAM ADS

Header Ads

WASANII SAIDA KAROLI KUTOKA TANZANIA NA OSOGO OWINYO KUTOKA KENYA WATUNISHIANA MISULI.

Majina haya, Saida Karoli kutoka Tanzania na Osogo Owinyo kutoka nchini Kenya, si Majina  mageni masikioni mwa wapenzi wa burudani katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki, Afrika na hata duniani kwa ujumla. Wasanii hawa kwa kipindi kirefu
wamedumu katika anga ya Mziki wa asili wanaoufanya na hivyo kuzidi kuwa kivutio kwa wapenzi wa burudani kila iitwapo leo.

Kwa Ukubwa wa Majina ya wasanii hao, ndiyo maana kila mmoja anachukuliwa kama atahitaji kuonyesha makali yake dhini ya mwenzake. Nadhani hujanielewa vizuri. Sasa kaa Mkao wa Kusoma kwa Umakini ili unielewe vyema. Saida Karoli na Osogo Owinyo leo tarehe 01.08.2014 Watakuwa wakitunishiana Misuli katika Jukwaa moja ndani ya Ukumbi wa Serengeti uliopo katika Hotel ya JB Belmont Jijini Mwanza katika Show kubwa kabisa iliyopewa jina la USIKU WA MWAFRIKA.
Kiingilio katika Show hiyo itakuwa ni shilingi 20,000 kwa VIP na shilingi 10,000 kwa viti vya kawaida. Katika Show hiyo wapenzi wa burudani watafaidi burudani kali kutoka kwa wasanii hayo huku wakisindikizwa pia na burudani ya kukata na shoka kutoka kwa Madancers wakali kutoka inchini Kenya wanaofahamika kama Chipukizi.Com. Zaidi utapata Misosi ya Kiafrika na Burudani za kiafrika. Atakaependeza kiafrika zaidi pia atapata zawadi. Kumbuka Milango inaanza kufunguliwa kuanzia saa moja jioni.
Hatimae burudani pia itahamia katika Viwanja vya Buzuruga Plaza siku ya Kesho ya tarehe 02.08.2014 kwa kiingilio cha shilingi 10,000 ambapo burudani kabambe itatolewa katika viwanja hivyo lengo likiwa ni kutoa burudani za kiafrika kwa Wakazi wa Jiji la Mwanza na Vitongoji vyake. Kumbuka ni Usiku wa Mwafrika, Burudani za Kiafrika na Misosi ya Kiafrika, hivyo hata wewe Ukitokelezea Kiafrika utakuwa Umetisha sana na utaweza kujipatia Zawadi kedekede.
"Tarehe hiiiii.....Mojaaaaaaa.......yaani....Mojaaaaaaaa" Hakika Saida Karoli kutoka Tanzania na Osogo Owinyo kutoka Kenya, ndani ya Jukwaa moja itakuwa ni zaidi ya Kutunishiana Misuli katika anga la Burudani. Hautakiwi kukosa.
Saida Karoli na Timu yake akishow love na mashabiki zake ndani ya 99.4 Metro FM Jijini Mwanza.
TAZAMA TANGAZO HAPA.

Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.