LIVE STREAM ADS

Header Ads

KUHADITHIA MIMI HUWA SIWEZI. TAZAMA MWENYEWE SHOW YA USIKU WA MWAFRIKA NDANI YA JB BELMONT HOTEL.

Show ya Usiku wa Mwafrika ndani ya JB Belmont Hotel Jijini Mwanza iliyopigwa jana tarehe 01.08.2014 imeacha gumzo kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na Vitongoji vyake, huku wengi wao wakibaki wanasimuliana namna
Wasanii wa Mziki wa Asili wanavyoweza kulimiliki Jukwaa. Wasanii waliotumbuiza katika Show hiyo ni Saida Kalori kutoka Tanzania, Osogo Owinyo kutoka Kenya na Wacheza Show wanao fahamika kama DotCom Chipukizi kutoka Kenya Pia pia. Pia kulikuwepo na Misosi ya Kiafrika ambapo kiingilio ilikuwa 20,000 VIP na 10,000 viti vya kawaida. Usiku wa mwafrika leo tarehe 02.08.2014 unahamia katika Viwanja vya Buzuruga Plaza kwa kiingilio cha shilingi 10,000.
Wacheza Show wa Osogo Owinyo Wakiwajibika Jukwaani. Hawa watu ni hatari tupu.
Wacheza Show wa Saida Kalori wakiwajibika Jukwaani. Ilikuwa balaa tupu.
Saida Kalori (Katikati) akiwajibika na wacheza show wake.
Wacheza Show wa Saida Kalori wakiwajibika.
Mwimbaji Saida Saida Kalori (Katikati) akiwa na Dancers wake wakiwa Jukwanii. Kiukweli walitoa Burudani iliyokidhi haja ya Wapenzi wa burudani.
Kulia ni Mwimbaji Osogo Owinyo kutoka nchini Kenya akitumbuiza Jukwaani.
Mwimbaji Osogo Owinyo kutoka nchini Kenya akitumbuiza Jukwaani.
Dancers wa Saida Kalori wakiwa Jukwaani.
Jikoni ilikuwa ni Kiafrika Zaidi.
Oxs Okeleky kutoka Radio Metro akifanya kitu roho inapenda.
Hii nayo ilikuwepo pia.
Misosi ya Kiafrika Ilikuwepo...Naona hapo Kichuri....Senene nk.
Oxs Okeleky kutoka Radio Metro (Kulia) akishow Love na Event Cordinator, Manta (Katikati) na Mwalimu wa Kundi la DotCom Chipukizi kutoka Kenya.
Mamaa Lonah (Kushoto) & Sefroza Joseph (Kulia) wote kutoka Radio Metro.
Taswira ya Ukumbini...Shughuli ilikuwa si Mchezo.
Hawa ndio walioingia katika Mchuano wa Kumtafuta alievaa Kiafrika Zaidi.
Mwakilishi kutoka DSTV (Katikati) akimkabidhi zawadi Mshindi wa Kwanza ambae alitokelezea Kiafrika katika Show hiyo ya Usiku wa Mwafrika iliyofanyika ndani ya JB Belmont Jijini Mwanza. Mshindi huyu alijishindia Dishi la DSTV.
Sefroza Joseph, Mwakilishi kutoka Radio Metro (Kushoto) akinena na Mshindi wa Kwanza ambae alivaa Kiafrika Zaidi na kumuahidi kuwa Radio Metro inampa nafasi ya kutangaza Biashara yoyote aliyonayo kwa muda wa Juma Moja sanjari na kutembelea katika Studio za Metro FM Jijini Mwanza kujionea Utendaji kazi wa Studio hiyo.
Frank M.Joackim (Mc wa Shughuli) kwa niaba ya Cocacola akimkabidhi zawadi Mshindi wa Pili alievaa Kiafrika.

Mwakilishi kutoka K Vant (Kushoto) akimkabidhi zawadi yake mshindi wa tatu ambae alivaa Kiafrika.
George Binagi, Mwakilishi kutoka Radio Metro (Kushoto) Akimkabidhi zawadi yake Mshindi wa Nne alievaa Kiafrika.
Philemon Tei ambae ni Meneja wa JB Belmont Hotel Jijini Mwanza (Kulia) akiwatambua washindia wa kudance waliodance vizuri ambapo wamepata nafasi ya kupata msosi mtamu katika Hotel hiyo.

K Vant nao walikuwa wakihakikisha kuwa kila anaeingia ukumbini anatapata radha ya kinywaji akipendacho.
Mapokezi napo kulikuwa na Ukarimu wa Kutosha.
Dancers wa DotCom Chipukizi kutoka nchini Kenya, pia walitisha kwa show kali.
 Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.