LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERENGETI FIESTA 2014 KWA MARA YA KWANZA JIJINI MWANZA...NI SHIDAAA!

Tarehe 09.08.2014 Kwa Mara ya Kwanza wananchi na wakazi wa Jiji la Mwanza na Maeneo Jirani
wanatarajia kupata burudani ya kukata na Shoka katika Uwanja wa CCM Kirumba. Hapa naizungumzia Show ya Serengeti Fiesta 2014 ambayo Mwaka huu inaanzia Kanda ya Ziwa katika Jiji lenye Miaka, kwa Maana ya Rock City Mwanza-Mwanza.

Kwa wapenda Burudani Kanda ya Ziwa, hii itakuwa ni fursa nyingine kwao kuweza kujumuika pamoja kwa ajili ya kushuhudia Burudani ambayo inatarajiwa kudondoshwa na Wasanii Wakali katika Jukwaa Moja la Serengeti Fiesta 2014 katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, huku homa ikiwa inazidi kupata kwa Wapenda Burudani wa Jiji la Mwanza ambao wanaisubiri show hiyo kwa hamu kubwa. Kiingilio katika Shows zote za Fiesta 2014 itakuwa ni Shiling 5,000 tu. Hakika hutakiwi kukosa mtu wangu.

Tazama Ratiba Kamili ya Serengeti Fiesta 2014 katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa:

SIKILIZA HAPA TANGAZO LA SERENGETI FIESTA 2014:


TAZAMA HAPA WIMBO WA SERENGETI FIESTA:


Na Mhariri: Mtanzania Media Blog.

No comments:

Powered by Blogger.