LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERENGETI FIESTA 2014 MWANZA NI SHEEDA. JAMANI TAZAMA HAWA MABAUNSA WAKINANIHIIIII.

Hili ni Nyomi la Watu waliojitokeza kusambaza upendo katika show ya Serengeti Fiesta 2014 ambayo Utepe wake ulikatwa jana Mkoani Mwanza. Hakika Kila Msanii aliepanda Jukwaani alisambaza upendo vile ilivyostahili. Maraia kibao walijitokeza Kiukweli kushow Love.Tazama Picha ya Chini jinsi Mabaunsa walivyokuwa wakiwajibika ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
Mabaunsa walikuwa na kazi ya ziada ili kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda kama kilivyopangiliwa. Hapa mizuka ilikuwa imepamba kweli kweli si unajua tena mizuka ya Burudani ya Serengeti Fiesta 2014 tena. Utepe ulikatwa jana Kwa mara ya Kwanza Katika Uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza na kila alietoa buku tano (5,000) yake alitoka roho imesuuzika kabisa. "UMEONA MABAUNSA WALIVYOKUWA WAKINANIHIII...I MEAN WAKIWAJIBIKA" Kiukweli walifanya kazi ipasavyo.
Wasanii kibao, Jukwaa moja waliweza kupagawisha ipasavyo huku Ney wa Mitego na Diamond Platnum ambae jana pia alipata na Wema na Ant Ezekiel wakionekana kuzikonga nyoyo za wanamwanza ipasavyo. Msanii mwingine aliekuwa na amsha amsha za kutosha ni Stamna ambae nae kiukweli wanamwanza walimuelewa sana. Yote tisa, kumi kila msanii aliepanda Jukwaani jana alitisha kiukweli yaani alilitendea haki Jukwaa la Serengeti Fiesta 2014 Mkoani Mwanza jana.
Hakika Wana Mwanza wameukata Utepe wa Serengeti Fiesta 2014 vyema hivyo Mikoa inayofuata inapaswa kufuata nyao ili kuivunja rekodi iliyoonyeshwa na wanamwanza. Kiukweli Mikoa Mingine inapaswa kusambaza upendo kwa pamoja kama ambavyo Mwanza ilisambaza upendo vya kutosha. Yaani ilikuwa ni SHEEEEEDA!
Picha zote na Gsengo Blog.

No comments:

Powered by Blogger.