LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI MKUU WA TANZANIA MH. MIZENGO PINDA ATUNUKIWA TUZO.


Viongozi mbalimbali kutoka Mkoa wa Kagera wakiwa wamejipanga tayari kwa ajili ya kumlaki Mh.Pinda alipokuwa

akitembelea mabanda mbalimbali ya Maonyesho katika Kilele cha Maonyesho ya Nane Nane yaliyofanyika Nyamhongolo Mkoani Mwanza. Mikoa yote Sita ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Simiyu, Shinyanga, Mara, Geita, Kagera na Mwenyeji Mwanza ilishiriki katika Maonyesho hayo. Kitaifa Maonyesho hayo yalifanyika katika Uwanja wa Ngongo Mkoani Lindi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal alikuwa Mgeni Rasmi.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Peter Kayanza Pinda ametunukiwa tuzo ya Kuwa Mkulima bora hapa nchini kwa mwaka 2014, kutokana na juhudi zake anazozionyesha katika kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kilimo na ufugaji.

Mh.Pinda alitunukiwa Tuzo hiyo wiki iliyopita na wakulima kutoka Kanda ya Ziwa katika Kilele cha Maonyesho ya Wakulima Nane Nane yaliyofanyika kwa Kanda ya Ziwa Nyamhongolo Mkoani Mwanza ambapo Mh.Pinda alikuwa Mgeni rasmi katika Kilele cha Maadhimisho hayo.

Tuzo hiyo ya Mkulima bora imetolewa kwa mara ya kwanza tangu maadhimisho ya Wakulima nane nane yaanze kuadhimishwa Kanda ya Ziwa ambapo Mikoa yote Sita ya Kanda ya Ziwa hujumuika kwa pamoja katika kuonyesha bidhaa mbalimbali za kilimo, uvuvi, ufugaji na Ujasiriamali.


Wakati Mh.Pinda anakabidhiwa tuzo hiyo, tayari juhudi zake za kuhakikisha kilimo kinakuwa uti wa mgongo hapa nchini zimeanza kuonekana ambapo mara kadhaa amekuwa akisisitiza zaidi juu ya uboreshaji na upatikanaji wa zana bora za kilimo sanjari na elimu kwa wakulima na wafugaji hapa nchini ili kuendana na wakati na kuwa na kilimo na ufugaji wa kisasa ambao una tija zaidi.

Mbali na kufahamika zaidi kama mtoto wa Mkulima, Mh.pinda anapendelea zaidi ufugaji wa Nyuki ambapo hadi sasa anamiliki zaidi ya mizinga 2,000 ya nyuki mbali na shughuli nyingine za kilimo na ufugaji anazozifanya.


Akizungumza katika Maonyesho hayo, Mh.Pinda aliwasisitizia zaidi wawekezaji mbalimbali wanaohitaji kuweka hapa nchini, kufika Kanda ya Ziwa kwa kuwa Kanda ya Ziwa ndilo eneo pekee lililo bora kwa uwekezaji kwa hivi sasa hapa nchini, kutokana na fursa nyingi zinazopatikana Kanda ya Ziwa.

Aidha Mh.Pinda aliwasisitizia zaidi wakulima na wafugaji hapa nchini kuwa na kilimo na ufugaji wa Kisasa kuendana na nyakati, badala ya kukumbatia kilimo na ufugaji wa kizamani ambao kwa hivi sasa hauna tija yoyote huku akiahidi kwamba tayari amefanya mazungumzo na wawekezaji mbalimbali ili kuhakikisha kuwa pamoja na maeneo mengine hapa nchini, Kanda ya Ziwa inakuwa na Kiwanda cha kuunganisha zana za kilimo (Matrekta) ili kuwawezesha wakulima wa kanda ya Ziwa kupata zana bora za kilimo kwa ajili ya shughuli zao.
Mh.Pinda akijionea Mihogo aina ya Mkombozi katika Maonyesho hayo.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza akijionea Mkungu wa Ndizi Kutoka Mkoani Kagera.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Halifa Hidda (Katikati) akiwa na viongozi wengine waliofika katika Maonyesho ya Nane Nane Kanda ya Ziwa yaliyofanyika Nyamhongolo Mkoani Mwanza.
Waandishi wa Habari wakiwa katika Majukumu yao katika Maonyesho ya Nane Nane Kanda ya Ziwa.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza katika Maonyesho hayo ya Nane Nane Kanda ya Ziwa yaliyofanyika Nyamhongolo Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, Mtumishi wa Mungu Baraka Konisaga akitoa Maelekezo katika Maonyesho hayo.
"Maonyesho ya Nane Nane.....OYEEEEEEEEE!!!!!!!" Salamu kutoka kwa Mh.Pinda.
Agness Hiza (Kulia) ambae ni Afisa Mauzo Kutoka Kampuni ya TING akiwa na Peter Tadeus nae Kutoka TING walipopokuwa katika Maonyesho ya Nane Nane yaliyofanyika Nyamhongolo Mkoani Mwanza. Zaidi wanasema kuwa BADO OFA YA MSIMU WA NANE NANE inaendelea ambapo kwa hivi sasa King'amzi cha TING HD kinapatikana kwa shilingi 89,000 bila dishi huku king'amzi chenye dishi kikipatikana kwa shilingi 176,000. Ofahiyo itafikia tamati mwisho wa mwezi wa Nane. Ofisi zao ziko Kemondo Mtaa wa Bantu Mkabala na ofisi za shirika la nyumba la Taifa au piga simu namba 0658 38 70 21 Kwa Maelezo zaidi.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.