Akipiga Story ndani ya 99.4 Metro FM ya Jijini Mwanza hii
leo, Platnum amebainisha kuwa kwa mara ya Kwanza atashusha burudani kali kwa
wapenda burudani wa Mkoa wa Mwanza na Vitongoji vyake ikiwa ni katika Kufungua
Msimu Mpya wa Serengeti Fiesta 2014 kwa mara ya Kwanza kabisa ikiwa inaanzia
Kanda ya Ziwa ndani ya Mkoani Mwanza
Amesema kuwa siku zote alikuwa akipanda jukwaani na
madancers wane, lakini hii leo kwa mara ya kwanza atapanda jukwaaani na
madancers 10 na atatumbuiza ngoma yake ambayo amesema inafanya poa sana katika
ardhi ya Bongo kwa hivi sasa, ngoma ya mdogo mdogo.
|
No comments: