LIVE STREAM ADS

Header Ads

VYOMBO VYA HABARI MKOANI MWANZA LAWAMANI.

Mwenyekiti wa kikundi cha Kirumba Sanaa, Issa Katumba.
Wasanii wa Maigizo na Muziki wa kizazi kipya Mkoani Mwanza wamevilaumu vyombo vya habari hususan Redio na Runinga kwa kushindwa kucheza nyimbo na kuonesha tamthilia zao, ambapo wakati mwingine wamekuwa wakiwaomba fedha na baadhi ya wafanyakazi wa vyombo hivyo pindi wanapopeleka kazi zao.

Akizungumza Wiki hii, Mwenyekiti wa kikundi cha Kirumba Sanaa Kilichopo Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, Issa Katumba alisema wadhamini wamekuwa wakishindwa kudhamini tamthilia zenye kuelimisha hivyo wamekuwa wakitoa kipaumbele kwa vitu ambavyo havielemishi jamii.

Katumba alisema kikundi hicho cha maigizo kimekuwa kikipambana na kuhakikisha jamii inapata elimu kupitia kazi wanayoifanya lakini wamekuwa wakikabiliwa na ukata wa fedha jambo ambalo wameshindwa kufikia lengo wanalokusudia.

Hata hivyo alisema mpaka sasa wameisha kamilisha tamthilia ya Malimwengu itakayoanza kuonyeshwa kupitia vituo mbalimbali vya televisheni nchini na kuingizwa kwenye king`amzi cha Continetal namba 107 ili kuhakikisha watanzania wanajifunza.
“Hii tamthilia ina maudhui ya kitanzania ambayo mtazamaji atakae pata nafasi ya kuiona atajifunza mambo mengi ya mila na desturi za mwafrika anavyotakiwa kuishi na ninawaomba watanzania wenzangu kuutuunga mkono. Alisema Katumba na kuongeza

“Tamthilia hii imechezwa na wasanii chipukizi kutoka mkoa wa Mwanza, Kalenga Kiokote ambaye amecheza kama muhusika mkuu katika  tamthia hiyo ambapo aliigiza kama kama mtoto wa mtaani alionesha uwezo mkubwa sana na ambae anahitaji kusaidia,” alisema Katumba.
Mwenyekiti wa kikundi cha Kirumba Sanaa, Issa Katumba.
 Na: Prisca Japhes, Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.