 |
Jumla ya Washiriki 18 wa Miss Lake Zone wakiwa katika Picha ya Pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Rishor pamoja na Mkurugenzi Mkuu (Me) sanjari na Mkurugenzi Mtendaji (Ke).
|
Wadau mbalimbali wameshauriwa
kujitokeza kuwekeza katika huduma mbalimbali za kijamii ambazo ni pamoja na
Elimu sanjari na Afya, kwa lengo la kusaidia katika kuihudumia jamii kwa kuwa
bado huduma hizo upatikanaji wake ni wa kusua sua hapa nchini.
Ushauri huo
umetolewa hii leo Mkoani Mwanza na Leus Kibona ambae ni Mkurugenzi Mkuu wa
Shule ya Awali na Msingi Rishor iliyoko Tarafa ya Usagara Wilaya ya Misungwi
Mkoani Mwanza, baada ya kutembelewa na Washiriki wa Shindano la Urembo Kanda ya
Ziwa, Maarufu kama Miss Lake Zone 2014.
Kibona
alibainisha kuwa bado sekta ya elimu inasua sua hapa nchini hivyo ni vyema watu
wenye uwezo wakawekeza kwenye elimu kwa kujenga shule na vyuo mbalimbali vya
elimu kwa lengo la kusaidia upatikanaji wa elimu sanjari na kuinua kiwango cha
elimu hapa nchini.
Aidha
aliongeza kuwa huduma za kijamii kama vile Afya pia nazo pia zinahitajika hivyo
wadau mbambali wajitokeze kwa aajili ya kujenga vyuo vya Afya na Zahanati ili
kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya katika jamii hapa nchini.
Ili
kuonyesha ushiriki wake katika jamii, Shule ya Rishor imeazimia kutoa nafasi
mbili kwa wanafunzi walio katika mazingira magumu katika Tarafa ya Usagara kwa
ajili ya kuwasomesha bure, huku Mkurugenzi wa Shule hiyo akiahidi kuongeza
idadi ya kuwasomesha wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kadri uwezo
wake utakavyokuwa ukiongezeka.
Kuhusiana na
Shindano la Redd’s Miss Lake Zone 2014, Shule ya Rishor ni miongoni mwa
wadhamni waliojitokeza katika udhamni, ambapo Mkurugenzi wa Shule hiyo aliwasihi
washiriki wa Shindano la Miss Lake Zone kuzingania pia suala la elimu
ili kuweza kupata uelewa zaidi shughuli zao.



Kwa
upande
wao Washiriki wa Shindano hilo waliezea furaha yao baada ya kuchaguliwa
kuiwakilisha Mikoa yao ya Kanda ya Ziwa, ambapo kila Mkoa umetoa
Washiriki
watatu kwa ajili ya kujishiriki Shindano hilo la Miss Lake Zone
2014
na hivyo kufanya idadi ya washiriki wa shindano hilo kuwa 18 kutoka
Mikoa yote sita ya Kanda ya Ziwa ambapo kiingilio kimepangwa kuwa ni
shilingi 5,000, 10,000 na 30,000.
Aidha
washiriki hao pia waliishauri jamii ya Watanzania kuwekeza zaidi katika elimu
kwa kuwa kiwango cha elimu hapa nchini bado hakiridhishi, huku wakiongeza kuwa
wakazi wa Kanda ya Ziwa ikiwemo Mkoa wa Mwanza wajitokeze kwa wingi siku ya
Jumamosi Agost 30 katika Uwanja wa CCMK Kirumba ili kushuhudia shindano hilo la Miss Lake Zone 2014.
Kwa Upande
wake Flora Lauwo ambae ni muandaaji wa Shindano hilo kupitia kampuni yake ya
Flora Promotion alibainisha kuwa, Mshindi wa Kwanza atapata zawadi ya gari
yenye thamani ya shilingi Milioni Kumi, Mshindi wa Pili atajipatia zawadi
Bajaji yenye tahamani ya shilingi milioni nne, ambapo mshindi wa tatu atapata
fursa ya kusomeshwa huku mrembo mwenye kipaji akijishindia zawadi ya pikipiki
yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki sita sanjari na zawadi
mbalimbali kutoka kwa wadhamni.
Nae Benny Mwangi ambae ni Meneja wa Lenny Hotel iliyopo Mkoani Geita,
alieleza kuwa Lenny Hotel ilijitokeza kudhamini shindano hilo kwa lengo la
kuboresha mashindano hayo, huku akiongeza kuwa jamii inapaswa kubadili mtizamo
na kuachana na fikra potofu kuwa mashindano ya urembo ni uhuni. Lenny Hotel
katika udhamini wake imetoa zawadi ya gari yenye thamani ya shilingi Milioni
kumi kwa ajili ya mshindi wa kwanza
 |
Mtoto huyu alikuwa ni Kivutio cha Mamiss kutokana na namna alivyokuwa akijipanga katika kupiga picha na Mamiss. |
 |
Jamani huyu Mtoto ni mcheshi sana. Hapa alikuwa na Anko wake George Binagi-GB Pazzo kutoka Radio Metro, akiwa pia ni Managing Director wa Mtanzania Media. |
 |
Warembo wanaoshiriki Redd's Miss Lake Zone wakiwa na Lydia (Katikati) ambae ni Mwandishi wa habari kutoka Radio City FM Jijini Mwanza. |
 |
Leus Kibona (katikati) ambae ni Mkurugenzi Mkuu wa Rishor Pre & Primary School akizunguka shuleni hapo hii leo baada ya warimbwende kutembelea shule yake. |
 |
Wa kwanza ni Leus Kibona ambae ni Mkurugenzi Mkuu , akifuatiwa na Peris Kibona ambae ni Mkurugenzi Mtendaji, anaefuata aliesimama ni Seleman Mohamed ambae ni Msema, hao ni baadhi ya Viongozi wa Rishor Pri & Primary School na anaefuata aliekaa ni Flora Lauwo ambae ni Mkurugenzi wa Flora Promotion, ambao ni waandaaji wa Mashindano ya Miss Lake Zone 2014. |
 |
Warimbwende wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Lake Zone 2014 |
 |
Wanafunzi wa Rishor Pri & Primary school |
 |
Ilikuwa Time ya Bites kidogo. |
 |
"Kasema nani kuwa Mamiss hawaliiiiiiii" Haya sasa sahani hizo hapo" |
 |
Wanafunzi |
 |
"Eti Kidoti akawa ananikiss, jamani majaribu mengine me siyawezi" |
 |
Flora Lauwo ambae ni Mwandaaji wa Redd's Miss Lake Zone 2014, chini ya Kampuni yake ya Flora Promotion. |
 |
Judith Josephat Maturege (Ke) ambae ni Matron wa Mamiis hao. |
 |
"Warimbwende" |
 |
Baadhi ya Majengo yaliyopo Rishor Pri & Primary School |
 |
Jengo la Utawala katika Shule ya Rishor Pri & Primary School likiwa na Vifaa vya Kisasa kabisa ndani yake. Shule hii ni ya Kutwa na Bweni. |
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.
No comments: