LIVE STREAM ADS

Header Ads

DAR ES SALAAM INSTITUTE OF JOURNALISM KUTOA MAFUNZO KWA WANAHABARI MKOANI MWANZA.

Wanafunzi wa Dar es Salaam Institute Of Journalism and Mass Communication Tawi la Mwanza.

Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication Tawi la Mwanza, kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza kimeandaa mafunzo kwa wanahabari kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wao.

Mafunzo hayo ambayo yamewalenga
waandishi wa Habari kutoka Mkoani Mwanza yamepangwa kutolewa kwa wanahabari ambao tayari wanajishughulisha na taaluma hiyo kwa uzoefu tu huku wakiwa hawana mafunzo yoyote kutoka taasisi yoyote inayotoa mafunzo hayo.
Wanafunzi wa Dar es Salaam Institute Of Journalism and Mass Communication Tawi la Mwanza.

Mbali na hao pia Wanahabari wengine wamepewa fursa ya kupata mafunzo hayo kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi katika shughuli zao za uandishi wa habari na utangazaji, ambapo mafunzo hayo yatatolewa katika kipindi cha Miezi Mitatu kuanzia Septemba 15 hadi Desemba 15 Mwaka huu.

Jasson Wambele ambae ni Meneja wa Chuo hicho cha Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication Tawi la Mwanza, ameeleza kuwa waandishi watakaopata mafunzo hayo wataweza kupatiwa vyeti na ametoa rai kwa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari Mkoani Mwanza kujiandikisha katika ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza kwa ajili ya kupata mafunzo hayo.
Wanafunzi wa Dar es Salaam Institute Of Journalism and Mass Communication Tawi la Mwanza wakiwa darasani.

Wambele amesema kuwa usaili tayari umeanza kufanyika katika Ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza zilizopo jengo la CCM Mkoa wa Mwanza ghoroma ya nne na kwamba mafunzo hayo yatatolewa kwa washiriki kuchangia gharama kidogo kiasi cha shilingi Laki Moja na Nusu (150,000) ambapo kiasi hicho kitalipwa kwa awali. Kila Mwezi shilingi Elfu Hamsini Tu (50,000)
Baadhi ya wanafunzi wa Dar es Salaam Institute Of Journalism and Mass Communication Tawi la Mwanza.
Mwalimu wa Dar es Salaam Institute Of Journalism and Mass Communication Tawi la Mwanza akipiga pindi chuoni hapo.
Dar es Salaam Institute Of Journalism and Mass Communication Tawi la Mwanza (wawili kulia) wakiwa na wanafunzi wa Chuo hicho (Wawili kushoto) katika majengo ya chuo hicho yaliyo Mkabala na Majengo ya Nyakahoja Jijini Mwanza.
Watumishi wa Dar es Salaam Institute Of Journalism and Mass Communication Tawi la Mwanza.
Jasson Wambele ambae ni Meneja wa Dar es Salaam Institute Of Journalism and Mass Communication Tawi la Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.