HII NI FAIDA NYINGINE YA DARAJA LA MABATINI JIJINI MWANZA.
![]() |
Taswira ya daraja la Mabatini.Hii ilikuwa Mapema wakati ujenzi ukiendelea. |
Baadhi ya
wakazi wa jiji la Mwanza wamesema kuwa pamoja na daraja la mabatini kuwa
msaada
mkubwa kwao utokana na kupunguza ajali zilizokuwa zikitokea mara kwa mara
katika eneo la Mabatini, pia daraja hilo limekuwa ni sehemu ya ajira kwao hususani
kwa vijana wanaojishughulisha na shughuli ya upigaji picha.
Baadhi ya vijana
wanaopiga picha katika eneo hilo wameleza kuwa, uwepo wa daraja hilo umeleta
ahueni kwao na hivyo daraja hilo kutokana na daraja hilo kuwa sehemu mojawapo
ya kujipatia kipato halali.
Jumanne Mbase ambaye ni mmoja wa wapigapicha katika daraja hilo
alieleza kuwa, baada ya kuona daraja limekamilika, aliamua kuanzisha shughuli
zake katika eneo hilo jambo ambalo lilimwongezea kipato zaidi tofauti na
alivyokuwa hapo awali.
“Nilianza kazi hii darajani hapa mwezi wa Machi mwaka
huu na kazi inaenda vizuri kwani kipato cha chini ninachopata kwa siku ni
shilingi 5000 na siku kazi ikienda vizuri Napata shilingi elfu kumi hadi elfu
kumi na mbili kwa siku..” Alieleza Jumanne.
Nae Jackson Jovin alieleza kwamba pamoja na wao kujiajiri mahali
hapo, pia wamekuwa ni msaada katika kuhakikisha eneo hilo linakuwa salama
wakati wote kwani kwa uwepo wao hapo wamekuwa wakililinda eneo hilo
kwa namna moja ama nyingine.
“Hatukai hapa kwa kupiga picha tu, bali tunaangalia usalama wa
eneo hili kwa ujumla, wakati mwingine walinzi wanakuwa wamekaa huko chini na
sisi tunapokuwa huku juu tunabeba jukumu la kuangalia usalama wa daraja hili.
Walieleza kuwa wapo baadhi ya watu ambao hufia katika daraja hilo
na kutaka kufungua baadhi ya nati na wengine kukwangua kwa kutumi vitu vyenye
ncha kali lakini wamekuwa wakidhibiti uharifu huo.
Wapigapicha wengine waliokuwa katika eneo hilo ambao ni Yohana
Daud na Isack Musa walieleza kuwa , ni vema jamii ikatambua jinsi ya kujitafutia
kipato, na sio kusubiri ajira kutoka serikalini huku wengine wakiishi amitaani
kuvuta bangi.
Daraja hilo lilijengwa kutokana na eneo hilo kuwa na msongamano wa
watu na magari, hivyo liliwekwa ili kupunguza ajari na vifo vilivyokuwa
vikitokea mara kwa mara katika eneo hilo.
Na Prisca Japhen-Mtanzania Media.
No comments: