LIVE STREAM ADS

Header Ads

OJADACT YATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI MKOANI MWANZA.

Wanahabari waliopata Mafunzo Mkoani Mwanza wakiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa OJADACT. 

Chama cha Waandishi wa Habari wanaopinga Madawa ya Kulevya na Uharifu nchini OJADACT,  hii leo kimetoa Mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza yenye lengo Kuwajengea Uwezo wa kuandika habari mbalimbali za kupambana na Madawa ya Kulevya Sanjari na Uharifu hapa nchini.


Mafunzo hayo ambayo
yametolewa kwa waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari Mkoani Mwanza, yamehusisha pia uwasilishaji wa Mada na Majadiliano, ambapo Mada zilizowasilishwa ni Maadili katika Uandishi wa Habari, sera na sheria za dawa sanjari na hali ya tatizo la dawa za kulevya ilivyo hapa nchini.
Viongozi wa OJADACT wakiwa katika Picha ya Pamoja.


Akifungua Mafunzo hayo ambayo yalikuwa ni ya siku moja, Edwin Soko ambae ni Mwenyekiti wa OJADACT alibainisha kuwa bado hali ya Matumizi, Uingizaji na Usafirishaji wa dawa za kulevya hapa nchini si shwari ambapo takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania inaongoza katika Ukanda wa Afrika Mashariki katika uingizwaji na usafirishaji wa dawa za kulevya huku pia idadi ya Watanzania wanaokamatwa na dawa hizo ikiwa kubwa.


Soko alisema kuwa Takwimu zinaonyesha kwamba kwa kipindi cha mwezi January hadi mwezi June mwaka huu, zaidi ya tani mbili ya shehena ya dawa za kulevya ilikamatwa huku Watanzania takribani 408 wakikamatwa na dawa za kulevya huko Ughaibuni.
Isaack Wakuganda ambae ni Gender Officer OJADACT.

Kutokana na Takwimu hizo, Soko alioongeza kuwa OJADACT imeona ni vyema ikaandaa mafunzo kwa Waandishi wa Habari, ili kuwajengea Uwezo wa kuweza kuandika habari zinazohusiana na dawa na kulevya pamoja na uharifu ili kufikisha elimu zaidi katika jamii.


Katika hatua nyingine Soko alibainisha kuwa kuna madhara makubwa yanayotokana na biashara na matumizi ya dawa za kulevya ambapo ameyataja madhara hayo kuwa yamegawanyika katika Nyanja mbalimbali ambazo ni pamoja na Kiuchumi, Kiafya, Kisiasa, Kijamii, Kiusalama na Kimazingira pia ambapo madhara yote hayo yana athari kubwa katika Mstakabali wa Taifa.

Akitoa Mada juu ya Uharifu katika Mitandao, Masaga Francis Mturi kutoka Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza alibainisha kuwa Waandishi wana nafasi kubwa ya kuilemisha jamii kwa uharaka zaidi na hivyo kuwaasa waandishi kuyatumia vyema mafunzo hayo kwa ajili ya kufikisha elimu ya kupambana na dawa za kulevya na uharifu katika jamii.

Kuhusiana na Suala la Uharifu katika Mtandao, Mturi alifafanua kwamba bado kuna changamoto kubwa kwani bado vyombo vya dola havijawa na uwezo wa kuweza kuzuia uharifu wa kimtandao huku akibainisha kuwa asilimia kubwa ya kesi zinazoripotiwa kutokana na wizi wa kimtandao, ni kesi chache ambazo vyombo vya dola hufanikiwa kuzishughulikia

Akiwasilisha Mada juu ya Maadili katika Uandishi, Dennis Mpagaze ambae ni Katibu wa OJADACT alibainisha kwamba vita na mapambano ya Dawa za kulevya inaonekana kuwa ngumu maana ni vita ambayo inahusisha mapambano na watu wenge nguvu kifedha na hata kimamlaka jambo ambalo limekuwa likikwamisha biashara biashara na matumizi ya dawa za kulevya kufanikiwa.

Alioongeza kuwa kwa nyakati tofauti baadhi ya watu wamekuwa wakitajwa hadharani kujihusisha na biashara hiyo lakini wamekuwa hawachukuliwi hatua yoyote jambo ambalo linatafsirika kwamba hata vyombo vya dola vimekuwa vikiteteleka katika mapambano ya dawa za kulevya.
Edwin Soko ambae ni Mwenyekiti wa OJADACT
Edwin Soko Mwenyekiti OJADACT (Kushoto) akiwa na Denis Mpagaze (Kulia) ambae ni Katibu OJADACT.
Aika Mboya ambae ni Mratibu wa OJADACT (Kushoto) akiwa na Shan Amanzi (Kulia) ambae ni Gender Officer OJADACT.
Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza wakiwa katika Mafunzo yaliyoandaliwa na OJADACT kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika habari zitakazosaidia mapambano dhini ya dawa za kulenya na uharifu nchini.
Mafunzo hayo yameratibiwa na OJADACT na Kufadhiriwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA.

No comments:

Powered by Blogger.