LIVE STREAM ADS

Header Ads

MSANII ELIZAYO HB KUTOKA ROCK CITY AWAUMIZA VICHWA WASANII WAKUBWA NCHINI.

Msanii Elizayo HB kutoka Rock City-Mwanza.
Msanii wa Kizazi kipya kutoka Rock City anaefahamika kwa jina la Elizayo FB amekuwa mwiba mkali baada ya kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Sina Raha ambao Umepikwa na Maproducer wawili wakali kinomanoma Kutoka Roct City ambao ni P'Silla na Kazi Moto huku ngoma hiyo ikipikiwa Silica Music Studio.

Baada ya Ngoma hiyo kuachiwa
imeonekana kuwashtua Watu wengi wakubwa Jijini Mwanza huku baadhi ya wasanii hao wakionekana kushtushwa na ujio wa Elizayo HB ambapo asilimia kubwa ya wasanii hao wamefurahishwa na uimbaji wake ambapo wamebainisha kuwa Msanii huyo aliiendelea na kasi aliyokuja nayo basi atakuwa tishio kimsiki hadi kwa wasanii wengine wakubwa nchini.

"Mimi namshukuru Mungu ngoma yangu imepokelewa vyema japo bado naona safari ni ndefu kwani nahitaji kufika mbali zaidi kimziki. Japo hatua niliyofikia kwa sasa si mbaya lakini nahitaji support zaidi maana nimefika hapa kwa nguvu zangu mwenyewe hivyo nikipata meneja kwa ajili ya kumeneji kazi zangu kiukweli nitatisha sana kimziki" Alisema Elizayo HB wakati akipiga story na Mtanzania Media.

ISIKILIZE NGOMA HIYO HAPA CHINI. MAWASILIANO 0752 61 38 70

No comments:

Powered by Blogger.