LIVE STREAM ADS

Header Ads

MBARONI KWA KUHUSIKA NA UVAMIZI WA KITUO CHA POLISI MKOANI GEITA.

KAMANDA WA POLISI MKOANI GEITA JOSEPH  KONYO.

Kufuatia msako mkali  uliofanywa jana na jeshi la polisi nchini katika Mkoa wa Geita  eneo la Ushirombo wilaya ya Bukombe, Jeshi hilo  limefanikiwa
kumkamata mtu mmoja waliyekuwa wakimhisi kuwa ni jambazi ambaye amekutwa akiwa ameketi juu ya mti huku akiwa ameshikilia bomu.

Mtu huyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja alikutwa juu ya mti majira ya jana jioni wakati msako mkali wa jeshi la polisi ukiendelea katika eneo hilo ambapo pia jeshi hilo limefanikiwa kupata bunduki saba aina ya SMG zikiwa zimefichwa kwenye tanuru la kuchomea matofali.

Jeshi la polisi pia lilimkamata mtu huyo huku likimficha sura yake kwa kitambaa cheusi baada ya kumhisi kuwa alishiriki kitendo cha mauaji ya askari wawili   waliokuwa zamu katika kituo kidogo cha polisi na watatu kujeruhiwa huku taarifa zikieleza kuwa askari mmoja aliyekuwa majeruhi alifia njiani wakati akikimbizwa katika hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza.

Hata hivyo jeshi la polisi nchini limetangaza dau  la shilingi millioni 10 kwa mtu yeyote atakaye fanikisha kuwakamata au kuwabaini waliohusika na uvamizi huo

Kituo kidogo cha polisi kilichopo ushirombo wilayani Bukombe  mkoani Geita  kilivamiwa  na majambazi usiku wa kuamkia jana jumamosi saa tisa usiku huku  askari wawili wakiuwawa na watatu wakijeruhiwa  vibaya.

Ambapo taarifa zilieleza kwamba kuwa majambazi hao walilipua  chumba cha kuhifadhia silaha  na kufanikiwa kuondoka na  silaha zaidi ya tano  aina ya SMG.

No comments:

Powered by Blogger.