LIVE STREAM ADS

Header Ads

MTANGAZAJI NGURI WA HABARI ZA MICHEZO MKOANI MWANZA, WAKUGANDA ATANGAZA RASMI KUACHA KAZI RADIO METRO.

Isaack Wakuganda ambae Alikuwa Mtangazaji wa Radio Metro ya Jijini Mwanza. Hapa alikuwa katika Studio za Metro Fm.

Mtangazaji na Mwandishi Mahili wa Habari za Michezo Mkoani Mwanza Isaack Wakuganda ambae alikuwa anafanya kazi na Kituo cha Radio Jijini Mwanza kinachofahamika kama Radio Metro ametangaza rasmi kuacha kazi katika kituo hicho.


Mtangazaji huo mwenye mbwembwe kweli kweli anapokuwa
kwenye kipindi ameweka bayana hii leo kuwa ameacha kazi katika kituo hicho huku akishindwa kuweka bayana sababu zilizopelekea yeye kuacha kazi katika kituo hicho cha Radio Metro ambacho ni gumzo katika Ukanda wa Ziwa.
Isaack Wakuganda (Kulia) akiwa na Sefroza Joseph wakati wakifanya kazi wote Radio Metro.

“Tarehe 03/09/2014 siku ya jumatano, nimeacha rasmi kazi ya utangazaji wa Michezo -Radio Metro FM ya Mwanza. Nimekitumikia kituo hicho kwa miaka mitatu toka mwaka 2011. Nawashukuru sana viongozi wa vyama vya michezo mbalimbali wa kitaifa, Mkoa wa Mwanza na Mikoa yote ya kanda ya ziwa bila kusahau viongozi wa vilabu vya soka Mkoani Mwanza kwa ushirikiano wao walioutoa kwangu. Sitawasahau wasikilizaji wangu, nawathamini sana. Michezo naipenda sana na hivyo nitaendelea kuwa mwanamichezo”. Alisema Wakuganda ambae wengi wanamfahamu kama Libero asiechoka anapokuwa dimbani.


Hatua hiyo ya Wakuganda kuacha kazi imeonekana kuwashtua watu wengi ndani na nje ya Jiji la Mwanza si tu kwa wasikilizaji wa Radio Metro bali hata pia takribani viongozi mbalimbali wa Vyama Soka hapa nchini ambao alikuwa akishirikiana nao kwa ukaribu zaidi.
Isaack Wakuganda (Wa kwanza Kulia) akiwa na Sefroza Joseph (Wa kwanza kushoto) na katikati ni Oxs Okeleky ambae ni Mtangazaji na Producer wa Metro Fm wakati wakifanya kazi wote Radio Metro.


“Bila shaka kuna fursa nyingine imetokea maana tunaishi kwa kuangalia wapi pa kupenya” Alisema mmoja wa Wasikilizaji wa Wakuganda huku mwingine nae akionekana kupigwa na butwaa baada ya kupata taarifa hizi “Atiiiiiiiiiiiiii sijaelewa”.


Mbali na Isaack Wakuganda kutokuwa tayari kuweka bayana sababu zilizosababisha yeye kuacha kazi  Radio Metro, Pia hajabainisha kwa hivi sasa atakwenda kufanya kazi na Chombo gani cha habari. Mbali na Kazi ya Utangazaji na Uandishi wa Habari, Wakuganda pia ni Mwalimu wa Shule ya Upili Mkolani iliyoko Jijini Mwanza.
Isaack Wakuganda (Kulia) akifanya Mahojiano na Mmoja wa Viongozi wa Soka Mkoani Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.