LIVE STREAM ADS

Header Ads

MBUNGE WA ILEMELA ASAFIRISHWA KWENDA INDIA KWA AJILI YA MATIBABU.

Wananchi na Wakazi wa Mkoa wa Mwanza waliofurika jana katika Uwanja wa Mbugani Wilayani Nyamagana katika Mkutano wa Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ambao ni Naibu Katibu Mkuu Bara Mh.John Mnyika pamoja na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu. Pia Viongozi mbalimbali wa Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA walihudhuria katika Mkutano huo.
Hali ya kiafya ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza (Chadema) Highness Kiwia imeelezwa kuwa mbaya ambapo Mbunge huyo amesafirishwa kwenda nchini India kwa ajili ya Matibabu zaidi.

Hayo yalibainishwa jana na
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (Chadema) Ezekiel Wenje katika Mkutano wa hadhara wa Chadema uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani Jijini Mwanza, ambao pia ulihudhuriwa na viongozi wa Kitaifa wa Chama hicho.

"...Hali ya Mbunge wenu Higness Kiwia si nzuri na usiku wa leo tunamsafirisha kwenda nchini India kwa ajili ya Matibabu.Kwa muda mrefu Kiwia amekuwa akisumbuka kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuvamiwa na kukatwa mapanga akiwa na wenzake ambapo baadhi ya mishipa yake ya usoni ilikatwa hali ambayo imesababishia ganzi katika uso wake kiasi kwamba hivi sasa hata ukimpiga ngumi hasikii chochote..." Alisema Wenje huku akiwataka wapiga kura wake kumuombea ili apate ahueni kwa jili ya kurejea ili aendelee kuwatumikia.

Wenje aliongeza kuwa kwa muda mrefu mbunge huyo amekuwa akisumbuliwa kutokana na majeraha aliyoyapata mwaka 2012 baada ya kuvamiwa na watu waliosadikiwa kutumwa kwa ajili ya kumuangamiza kutokana na itikadi zilizoelezwa kuwa ni za kisiasa akiwa na makada wengine wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
Wananchi wakiwa katika hali ya Utulivu wakiwasikiliza Viongozi wa Chadema waliokuwa wakihutubia katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Viongozi wa Kitaifa wa Chadema ambao ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Tanzania Bara John Mnyika na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Tanzania Visiwani Salum Mwalimu ambapo wote kwa pamoja walieleza kutounga Mkono Mchakato wa Katiba Mpya unavyoendeshwa na Mwenyekiti wa Bunge hilo Mh. Samwel Sitta.

Walieleza kwamba kitendo cha Sitta kuliongoza Bunge hilo kufanya marekebisho ya Sheria za upigaji kura katika Bunge hilo kwa kuwaruhusu wajumbe watakaokuwa nje ya bunge kupiga kura, ni mbinu cha za kutafuta kura kwa namna yoyote ile kwa ajili ya kuhakikisha kwamba theluthi mbili ya kura za wajumbe wa bunge hilo kutoka pande zote mbili za bara na visiwani inapatikana.
Wananchi waliofika katika Mkutano wa Chadema uliofanyika jana katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani Jijini Mwanza wakinyoosha Mikono juu kama ishara ya kuunga Mkono Kukataa Mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba linavyoendeshwa Mjini Dodoma ikiwa ni pamoja na Marekebisho ya Upigaji Kura wa wajumbe watakaokuwa nje ya Ukumbi wa Bunge hilo kupewa fursa ya Kupiga Kura.
Wananchi waliofika katika Mkutano wa Chadema uliofanyika jana katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani wakinyoosha vidole juu ikiwa ni ishara ya kukubaliana na kilichokuwa kikizungumzwa katika Mkutano huo.
Baadhi ya Viongozi wa Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA Mkoa wa Mwanza. Vyama hivyo ni Chadema, NCCR Mageuzi pamoja na CUF.
Viongozi mbalimbali wa Chadema.
Viongozi wa Chadema na CUF.
Naibu Katibu Mkuu Chadema kutoka Tanzania Visiwani Salum Mwalimu.
Naibu Katibu Mkuu Chadema Tanzania Bara John Mnyika.
Mnyika akiwa jukwaani ambapo alitaja hadharani namba za Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalumu la Katiba Andrew Chenge kwa lengo la kumpigia simu na kumueleza kuwa hawaungi Mkono Mapendekezo ya Katiba aliyoiwasilisha Bungeni kwa ajili ya Kupigiwa kura na Wajumbe wa Bunge hilo waliosalia bungeni.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (Chadema) Ezekiel Wenje (Alienyoosha Mkono juu).
Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.