LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAZAMA KILICHOJILI KATIKA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE IPWAGA SEKONDARI.

Wahitimu wa Kidato cha Nne kutoka Shule ya Sekondari Ipwaga iliyopo Usagara Wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza, wakiwa katika picha ya Pamoja na Mariam Lugayila (katikati waliokaa) ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Misungwi ambae alikuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali yao  pamoja na Mkuu wa Shule hiyo Mwl.Milambo Malegi (wa Pili Kulia waliokaa) na na viongozi wengine wa shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza Mariam Lugayila amewataka Vijana kujiepusha na Makundi mabaya katika jamii, ili kuondokana na tabia zinazoweza kuwaingiza katika mienendo isiyofaa ikiwemo kujiingiza katika usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya.

Lugayila aliyasema hayo
hii leo alipokuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Kidato cha Nne ya Wanafunzi wa Shule ya Ipwaga Sekondari iliyoko Usagara Wilayani Misungwi, yaliyofanyika katika viunga vya Shule hiyo.

Alisema vijana wanapaswa kuwa makini kwa kujiepusha na makundi hatarishi katika jamii ambayo yanaweza kuwaingiza katika suala la utumiaji au usafirishaji wa dawa za kulevya, jambo ambalo amesema ni hatari kwa kuwa linaweza kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

Aidha Lugayila aliwaonya vijana kujiepusha na suala la dawa za kulevya kwa kuwa wanaweza kupoteza maisha yao kama ambavyo baadhi ya nchi zimekuwa zikifanya kwa kutoa adhabu ya kifo kwa wale wanaokutwa wakijihusisha na utumiaji au usafirishaji wa dawa hizo.

Mbali na hayo Lugayila pia aliwataka mabinti kuzingatia zaidi masomo na kujiepusha na mimba za utotoni huku pia akiwakumbusha vijana wa kiume kujiepusha na mashuga mami jambo amablo litawawezesha kutimiza ndoto walizojiwekea katika maisha yao.
Picha ya Pamoja.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mariam Lugayila (Aliesimama) akizungumza katika Mahafali ya Kidato cha nne Shule ya Sekondari Ipwaga iliyoko Usagara Misungwi Mkoani Mwanza.
Wageni Waliikwa wakiwa pamoja na Mgeni Rasmi pamoja na Wakuu wa Sule ya Ipwaga Sekondari.

Wakuu wa Ipwaga Sekondari wakifurahia burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika Mahafali ya Kidato cha nne hii leo shuleni hapo.
Meza kuu ikiongozwa na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mariam Lugayila (Wa pili kulia).
Baadhi ya Wazazi waliohudhuria katika Mahafali ya Kidato cha Nne ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ipwaga iliyoko Usagara Wilayani Misungwi.
Baadhi ya Wazazi waliohudhuria katika Mahafali ya Kidato cha Nne ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ipwaga iliyoko Usagara Wilayani Misungwi.
Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Ipwaga Iliyoko Misungwi Mkoani Mwanza.
Add captionBaadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Ipwaga Iliyoko Misungwi Mkoani Mwanza.
Wahitimu wa Kidato cha Nne Ipwaga Sekondari.
Wahitimu wa Kidato cha Nne Ipwaga Sekondari.
Mmoja wa Wahitimu akipokea cheti (Si cheti halisi).
Mwalimu wa Ipwaga Sekondari akipata Motisha baada ya wanafunzi kufaulu vyema katika somo lake kulingana na Mitihani mbalimbali waliyoifanya.
Mwalimu wa Ipwaga Sekondari akipata Motisha baada ya wanafunzi kufaulu vyema katika somo lake kulingana na Mitihani mbalimbali waliyoifanya.
Mwalimu wa Ipwaga Sekondari akipata Motisha baada ya wanafunzi kufaulu vyema katika somo lake kulingana na Mitihani mbalimbali waliyoifanya.
Mwalimu wa Ipwaga Sekondari akipata Motisha baada ya wanafunzi kufaulu vyema katika somo lake kulingana na Mitihani mbalimbali waliyoifanya.
Mwalimu wa Ipwaga Sekondari akipata Motisha baada ya wanafunzi kufaulu vyema katika somo lake kulingana na Mitihani mbalimbali waliyoifanya.
Vaileth Elias (Kushoto) akiwa na Fadhir Jackson wakisoma Risala ya Wahitimu wa Kidato cha nne Ipwaga Sekondari katika Mahafali yao yaliyofanyika hii leo katika viwanja vya shule hiyo iliyoko Usagara Wilayani Misungwi.
Vaileth Elias akikabidhi Risala ya Wahitimu baada ya kumaliza kuisoma kwa Mgeni Rasmi.
Madam akiwakabidhi Keki wahitimu kama ishara ya upendo wake kwao haswa kutokana na nidhamu waliyonayo walihitmu hao.
Hakika nidhamu ni jambo la Busara. Baada ya wanafunzi wanaotarajiwa kuhitimu kuonyesha nidhamu ya hali ya juu, Madam wao akaamua kuwatengenezea Keki kwa ajili ya kuwatia moyo juu ya nidham waliyoionyesha.
Hawa ni washiriki wa Igizo ambalo lilikuwa na mafundisho tele ambapo lilikuwa likimhusisha mwanafunzi ambae alijiingiza katika mapenzi akiwa shuleni kutokana na tamaa za pesa na vitu mbalimbali kama simu na hatimae akajikuta akipachikwa mimba.
Hapa vijana wa Kizazi kipya walikuwa wakitoa burudani ya miondoko ya Hip Hop.
Hapa burudani ikiendelea ambapo wanafunzi wa kidato cha kwanza walitoa burudani ya ngoma za asili ili kutukumbuka kuwa bado Utamaduni wa Mtanzania na wa Kiafrika unapaswa kuenziwa.
Wanafunzi wa Ipwaga Sekondari wakitoa burudani katika Mahafali ya Kidato cha nne hii leo shuleni hapo.
Huyo Mshkaji katika gizo ametumia jina la Young Milionea, ni bingwa wa kuhonga balaa, lakini alivyomtundika mwanafunzi mimba alikuwa mpole kama mti ulionyauka na hatimae kumkimbia binti aliekuwa akimhadaa kwa pesa na simu. Wanafunzi wa kike kuweni makini na watu wa aina hii maana ni wengi mitaani.
Hapa mwanafunzi aliekuwa akijihusisha na mapenzi huku akiwa shuleni (Mwenye simu) ameenda kupima afya baada ya kuona hali inakuwa ndivyo sivyo ambapo alikutwa na mimba na hapo ndipo akachanganyikiwa kabisa. Ewe mwanafunzi kumbuka Mapenzi katika umri mdogo ni marufuku kwa masomo na afya yako.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa katika Mahafali ya Kidato cha Nne Ipwaga Sekondari iliyopo Mita chache Kutoka Usagara Conner Maarufu kama Round about ya Usagara.
Na: George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.