LIVE STREAM ADS

Header Ads

MEYA WA JIJI LA MWANZA AFUNGUA RASMI MAFUNZO KWA WANAHABARI MKOANI MWANZA.

Picha ya pamoja kati ya Mgeni Rasmi, Viongozi wa MPC, Viongozi na Walimu wa Chuo cha DIJ na Wanahabari wanaopata Mafunzo ya Tasnia ya Habari baada ya Uzinduzi Rasmi wa Mafunzo hayo hii leo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Shing'ong'o Mabula, amefungua rasmi Mafunzo ya Miezi Mitatu kwa Wanahabari Mkoani Mwanza, Mafunzo ambayo yanatolewa na Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es salaam Institute of Journalism (DIJ) tawi la Mwanza kwa ushirikiano na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza (MPC).

Akifungua mafunzo hayo
hii leo, Mabula alibainisha kuwa wanahabari wana nafasi kubwa ya kulibadilisha Taifa kimaendeleo, hivyo akawataka wanahabari wanaopata mafunzo hayo kuhakikisha wanayatumia vyema katika kulibadili Taifa kimaendeleo.

"Watu wanasema Taifa linaongozwa na wanasiasa. Mimi nasema wanahabari wana nafasi kubwa ya kuliongoza Taifa kwa kuwa wakiamua kulijenga wanaweza, na wakiamua kulibomoa wanaweza pia. Hivyo niwatake wanahabari wanopata mafunzo haya wahakikishe wanakwenda kuyatumia vyema mafunzo wanayoyapata katika kuliletea Taifa maendeleo". Alisema Mabula.

Kwa upande wake Jasson Wambele ambae ni Meneja wa Chuo cha Dar es salaam Institute of Journalism (DIJ) Tawi la Mwanza, alieleza kuwa, kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza walifanya utafiti na kugundua kwamba kuna wanahabari ambao wanafanya kazi ya uandishi wa habari kwa uzoefu bila kuwa na taaluma hiyo, hiyo wakaona ni vyema wakaandaa mafunzo hayo kwa ajili ya kuwajengea msingi wa taaluma ya habari waandishi hao huku wakitoa fursa pia kwa wanahabari wengine wenye taaluma ya habari kupata mafunzo hayo kwa lengo la kuwaimarisha zaidi.
Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mafunzo kwa Wanahabari Mkoani Mwanza, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Shing'ong'o Mabula akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo hii leo. Ufunguzi huo umefanyika katika Chuo cha Dar es Salaam Institute of Journalism & Mass Communication kilichopo katika Majengo ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Moshi Muccobs Jijini Mwanza.
Mafunzo hayo yanatolewa kuanzia saa 10 alasiri na yanatarajiwa kudumu kwa muda wa Miezi Mitatu ambapo washiriki wake wanachangia gharama kidogo kwa ajili ya uendeshaji wake, ambapo kila mshiriki anachangia shilingi Elfu Hamsini kwa Mwezi ambapo kwa miezi mitatu Kila Mshiriki atachangia kiasi cha shilingi Laki moja na Elfu hamsini tu.

Jumla ya wanahabari 50 Mkoani Mwanza walijiandikisha kupata mafunzo hayo, lakini Mpaka sasa waliojitokeza kwa ajili ya kupata mafunzo hayo wakiwa ni 30 pekee huku wengine wapatao 20 wakishindwa kuanza mafunzo hayo kwa minajili ya kushindwa kulipia mafunzo hayo licha ya gharama yake kushushwa ikilinganishwa na ada inayolipwa katika vyuo mbalimbali vinavyotoa mafunzo ya habari hapa nchini.

Kutokana na Changamoto hiyo kwa baadhi ya wanahabari walioshindwa kuchangia gharama za mafunzo hayo, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula aliwachangia gharama za mwezi mmoja wa kwanza ajili ya kuwawezesha wanahabari hao kujiunga na mafunzo hayo.

Wakizungumza na Mtanzaniamedia Blog, baadhi ya wanahabari wanaopata mafunzo hayo wameelezea kufurahishwa kwao na mafunzo hayo hususani katika somo la Kifaransa ambapo wameeleza kuwa wanatarajia kuongeza ujuzi mpya zaidi ambao utawawezesha kuyatenda vyema majukumu yao ya uandishi wa habari.
Stanslaus Mabula akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo kwa Wanahabari Mkoani Mwanza, Mafunzo ambayo yamelenga kuwajengea Uwezo zaidi wanahabari bila kujali wenye taaluma ya habari ama laa!
Jasson Wambele ambae ni Meneja wa Chuo cha Dar es salaam Institute Of Journalism (DIJ) Tawi la Mwanza akizungumza na Wanahabari baada ya uzinduzi wa Mafunzo kwa Wanahabari Mkoani Mwanza. Mafunzo hayo yalianza tangu Septemba 22 na yanatarajiwa kufikia tamati Desemba 22 ambapo washiriki wa Mafunzo hayo watatunukiwa Vyeti.
Jiimy Luhende Mwanahabari na Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza (MPC) akizungumza katika Ufunguzi huo hii leo.
Dotto Bulendu ambae ni Mwanahabari Mahiri, Mkurugenzi wa Radio Saut FM na Afisa Program kutoka Chama cha waandishi wa habari wanaopinga matumizi ya dawa za kulevya Mkoani Mwanza OJADACT wakati akizungumza hii leo katika Ufunguzi wa Mafunzo kwa Wanahabari Mkoani Mwanza.
Joseph Mlinzi ambae ni Afisa Habari Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Emmy Rehema akisoma Risala kwa niaba ya Wanahabari wanaopata Mafunzo ya Uandishi wa Habari Mkoani Mwanza.
Msoma Risala ya Wanahabari wanaopata Mafunzo ya Habari Mkoani Mwanza Emmy Rehema akikabidhi Risala kwa Mgeni Rasmi Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Shing'ng'o Mabula (Wa tatu kulia).
Meza kuu ikiongozwa na Mgeni Rasmi, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (Mwenye miwani) akinong'onezana jambo na Meneja wa DIJ Tawi la Mwanza Jasson Wambele (Wa pili Kulia).
Wanahabari wakifuatilia kwa umakini kabisa ufunguzi Rasmi wa Mafunzo ya Miezi Mitatu kwa wanahabari Mkoani Mwanza.
Wanahabari Wakongwe na Mahiri Mkoani Mwanza wakibadilishana Mawazo baada ya Ufunguzi Rasmi wa Mafunzo ya Miezi Mitatu kwa Wanahabari yanyotolewa na Chuo cha Dar es salaam Institute of Journalism & Mass Communication Tawi la Mwanza kwa ushirikiano wa Karibu kabisa na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC).
Na: George Binagi.

3 comments:

  1. kwa ujumla mafunzo haya yatawajenga wanahabari na kuboresha weledi wao wa habari

    ReplyDelete
  2. jason wambeleSeptember 27, 2014

    good news!!

    ReplyDelete
  3. Hii imekaa poa sana maana elimu haina mwisho

    ReplyDelete

Powered by Blogger.