LIVE STREAM ADS

Header Ads

MCHUNGAJI KILINGA ASIMIKWA KUWA ASKOFU MKUU WA KWANZA WA GOSHEN INLAND CURCH TANZANIA.

Askofu Charles Sekelwa (Katikati) kutoka Kanisa la Charismatic Epscopac Church (CEC) Kwa kushirikiana na Maaskofu wengine akimsimika Askofu Seleman Kilinga ambae alikuwa Mchungaji wa Kanisa la Goshen Island Church Kuwa Askofu Mkuu wa Kwanza wa Kanisa hilo nchini Tanzania. Sherehe za Kusimikwa kwa Askofu Kilinga zilifanyika jana katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabatini Jijini Mwanza ambapo sherehe hizo pia ziliambatana na Maadhimisho ya Miaka Kumi ya Kanisa hilo ambalo lilianzishwa Septemba 2004 likiwa na Makao Makuu yake Mabatini Jijini Mwanza.
Askofu Seleman Kilinga (Wa Kwanza Kushoto) akisimikwa kuwa Askofu wa Kwanza wa Kanisa la Goshen Inland Church.
Askofu Charles Sekelwa (Wa pili Kulia) kwa kushirikiana na Maaskofu wengine Watatu kutoka Makanisa ya Kipentekost wakimsimika Askofu Seleman Kilinga kuwa Askofu Mkuu wa Kwanza nchini Tanzania wa Kanisa la Goshen Inland Church lililopo Mabatini Jijini Mwanza katika Sherehe ambazo ziliambatana na Maadhimisho ya Miaka Kumi ya Kanisa hilo tangu kuanzishwa kwake Septemba Mwaka 2004.
Askofu Mkuu wa Kwanza nchini Tanzania wa Kanisa la Goshen Inland Church lenye Makao Makuu yake Mabatini Jijini Mwanza.
Askofu Kilinga akiwa na Mama Askofu (Mkewe) baada ya Kusimikwa siku ya jana.
Askofu Seleman Kilinga wa Kanisa la Goshen Inland Church (Wa tatu kutoka kila upande) akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekosti baada ya Kusimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Kwanza wa Kanisa hilo.
Viongozi wa Makanisa, Maaskofu na Wake za Maaskofu wakiwa katika Picha ya Pamoja.
Wachungaji wakiwa katika Picha ya Pamoja na Maaskofu.
Wazazi wakiwa katika Picha ya Pamoja na Maaskofu.
Kwaya ya Goshen Inland Church Mabatini ikiwa katika picha ya Pamoja na Maaskofu.
Kwaya ya Watoto kutoka Goshen Inland Church Mabatini wakiwa katika picha ya pamoja na Maskofu akiwemo Askofu Mkuu wa Kwanza wa Kanisa lA Goshen Inland Church Seleman Kilinga (Wa kwanza Waliokaa.)
Viongozi wa mbalimbali wa Kanisa.
Askofu Seleman Kilinga akiiwasili katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mabatini Jijini Mwanza kwa ajili ya Kusimikwa Rasmi kuwa Askofu Mkuu wa Kwanza wa Kanisa la Goshen Inland Church lenye Makao Makuu yake Mabitini Jijini Mwanza.
Waumini mbalimbali wakishuhudia Usimikaji wa Askofu Mkuu wa Kwanza wa nchini Tanzania wa Kanisa la Goshen Inland Church katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabatini siku ya jana.
Ahsante kwa Kutembela MTANZANIAMEDIA BLOG, Kwa Pamoja, Tuijuze Jamii.
Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.