LIVE STREAM ADS

Header Ads

MTOTO ATOWEKA GHAFLA MKOANI MWANZA. ANATAFUTWA NA NDUGU ZAKE.

Mtoto Ramadhan Nuru (11) Mkazi wa Mtaa wa Kabuhoro Kirumba.
 Mtoto Ramadhan Nuru (11) Mkazi wa Mtaa wa Kabuhoro Kirumba Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, anatafutwa na ndugu zake baada ya kutoweka nyumbani kwao tangu
Septemba 14 mwaka huu.


Mara ya Mwisho mtoto huyo mwenye jinsia ya Kiume alikuwa amevaa shati la drafuti lenye mikono mifupi likiwa na rangi nyeupe, na suruali yenye rangi ya ugoro pamoja na viatu vyenye rangi nyeusi.
Kwa yoyote atakae bahatika kumuona mtoto huyo anaombwa kutoa taarifa katika kituo chochote cha polisi kilicho karibu nae au awasiliane na baba wa mtoto huyo Nuru Barongo ama kaka zake na Mtoto huyo Amadi Amada na Mbaraka Nuru kwa nambari za simu 0688 27 22 28, 0683 59 58 25, 0768 42 39 74 na 0759 16 18 99.

Tafadhari unaombwa kutoa ushirikiano wako pindi utakapomuona mtoto huyo hususani maeneo ya Jijini Mwanza ambako inasadikiwa kwamba mtoto huyo ametolokea.
Taarifa hii imetolewa na ndugu zake.

No comments:

Powered by Blogger.