LIVE STREAM ADS

Header Ads

UKARABATI WA UWEKAJI NYASI BANDIA KATIKA UWANJA WA NYAMAGANA JIJINI MWANZA WAANZA.

Hayawi hayawi hatimae yamekuwa baada ya Kimya cha muda mrefu tangua Uwanja Mkongwe wa Nyamagana ulioko Mkoani Mwanza kuingizwa katika orodha ya Viwanja vya Shirikisho la Soka Duniani FIFA ili kuwekewa nyasi badia.

Baada ya Tathmini ya Muda mrefu katika Uwanja huo, hatimae Ukarabati wa kuuwekea nyasi za bandia Uwanja wa Nyamagana Umeanza siku ya
jana chini ya Kampuni ya Ujenzi ya Jassie and Company Limited ( JASCO) ambayo imepewa tenda ya ukarabati huo.

Ili kufanikisha zoezi hilo la Uwekaji wa nyasi bandia katika Uwanja huo wa Nyamagana, FIFA ilitoa kiasi cha dola za Marekani 500,000 ambapo Manispaa ya Jiji la Mwanza ambao ndiyo wamiliki wa uwanja huo, imechangia kiasi cha dola 118,000 (Sh milioni 295) kama mchango wake kwa ajili ya zoezi hilo ambalo linatarajiwa kugharimu dola 618,000 (Sh milioni 988).
Uwanja wa Nyamagana utakuwa ni uwanja wa nne kuwekewa nyasi hizo za bandia hapa nchini ambapo tayari viwanja vya Uhuru na Karume vya jijini Dar es Salaam na Migombani cha Zanzibar vimewekewa nyasi hizo huku Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera nao ukiwa ni Miongoni mwa Uwanja ulio katika orodha ya kuwekewa nyasi bandia na hivyo kuongeza idadi ya viwanja vyenye nyasi bandia hapa nchini.

“Hii ni nafasi nzuri kwa wana Mwanza kuhakikisha mchezo wa soka unarudi kwenye nafasi yake kwa kasi kama ilivyokuwa siku za nyuma nami niliahidi nilipofika mkoani hapa kuwa nitahakikisha michezo inakuwa kwenye nafasi nzuri.” Hiyo ilikuwa ni sehemu ya hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo wakati akitoa taarifa kwa wanahabari Mkoani Mwanza Miezi kadhaa iliyopita juu ya Ukarabati wa Uwanja huo.

Chama cha Soka Mkoani Mwanza MZFA kupitia kwa Mwenyekiti wake Jackson Manji Songora kimefurahishwa na Ukarabati wa Uwanja huo ambao unaonekana utaweza kuongeza chachu ya Kimichezo katika Mkoa wa Mwanza licha ya Mkoa huo kutokuwa na timu inayocheza ligi kuu Msimu huu baada ya Timu tegemewa za Toto African Fc na Pamba Fc juhudi zao za kurejea ligi kuu kutozaa matunda.
Hii ni mechi kati ya Simba na Yanga, iliyopigwa Uwanja wa Nyamagana mwaka 1974. Hapa kipa Athumani Mambosasa (marehemu) anaruka kudaka mpira mbele ya Kitwana Manara.
Na: George Binagi

No comments:

Powered by Blogger.