LIVE STREAM ADS

Header Ads

WIZI WAKITHIRI SOKO LA BUZURUGA WILAYA YA ILEMELA MKOANI MWANZA.

Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Buzuruga lililoko Wilaya ya ilemela Mkoani Mwanza,wamelalamikia uongozi wa soko hilo kutokana na hali wizi wa baadhi ya vitu na bidhaa  uliopo soko hapo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wafanyabiashara hao
wameeleza kuwa hali hiyo ya udokozi imekuwa ikiwaweka katika wakati mgumu kutokana na kupotelewa kwa bidhaa zao nyakati za usiku wanapoziacha na kuelekea majumbani mwao.

“Tumechoka na huu udokozi wa mali zetu, kila kukicha ni lazima mali zetu zipotee na tunashindwa kuelewa ni wapi zinapelekwa”alisema Ramadhani Hussen ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara waliopo katika soko hilo.

Alieleza kwamb, wamekuwa wakiacha biashara zao zikiwa salama na kamilifu, lakini wanaporudi kesho yake, baadhi yao wanakuta vitu vimepungua na hawaelewi ni kitugani kinavipunguza.

“Hili soko lina walinzi, lakini kila kukicha tunakuta baadhi ya vitu havipo, inakuwaje vinapotea wakati watu wa kuangalia usalama wa bidhaa zetu wapo na tunawalipa”?Alihoji Metusela Obedi ambae nae ni mfanyabishara sokoni hapo.

Akizungumza kuhusiana na kero hiyo ya wizi ambayo inawakabiri wafanyabiashara hao, Kaimu Mwenyekiti wa soko hilo Alfan Kazinza, alisema kuwa uongozi wa soko hilo unafanya kila jitihada ikiwa ni pamoja na  kuwashirikisha wafanyabiashara wa soko hilo kuhakikisha kuwa kero hiyo inatokomezwa ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha kutoa michango ya fedha itakayosaidia kupata ulinzi imara katika soko hilo.

Hata hivyo Kazinza aliiomba halmashauri ya wilaya ya Ilemela kupitia kwa Afisa masoko kuimarisha miundombinu ya soko  hilo, kwani hilo ndilo eneo muhimu la wananchi kujipatia kipato kwa ajili ya kuendesha maisha ya familia zao.
Na: Prisca Japhes

No comments:

Powered by Blogger.