WAUMINI NA VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI MKOANI GEITA WATAKIWA KUHAMASISHA AMANI.
Waumini
na Viongozi wa madhehebu mbalimbali Mkoani Geita wametakiwa kuhamasisha suala
zima la amani ya Taifa na Upendo katika Makanisa yao na jamii inayowazunguka kuhusu uchaguzi na mchakato wa upatikana kwa Katiba
Mpya.
Hayo yalisemwa juzi na Kamanda wa Umoja wa
vijana wa CCM wilaya ya
Nyan’gwale Mkoani Geita Idd Kassim,
wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa la The Evangelistc Assembles of God
Tanzania (EAGT).
Harambee hiyo iliyofanyika septemba 21 ilikuwa na lengo la kukusanya shilingi Millioni
9,970,000 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa
hilo ambapo kiasi cha pesa taslim kilichopatikana ni sh.Million
2,291,200 na mifuko 2 ya saruji huku ahadi ikiwa ni sh. Million 250,000 viti 7 na Mifuko 5 ya saruji.
Kassim alisema waumuni
wanatakiwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa na kutokubali kuoingiliwa kisiasa na wanasiasa wasiolitakia
mema taifa na kuchochea vurugu zisizo na
faida kwa watanzania.
“Tutambue hii ni nchi yetu sote na tunajukumu la kuilinda amani na
upendo uliopo, uendelee kuwepo”Alisema Kassim.
Aidha Kamanda Idd aliwataka vijana wa wilaya hiyo, kujiajiri wenyewe ili waweze kujiletea
maendeleo katika familia zao na kuepukana na janga la ukosefu wa ajira kwa
vijana.
Na: Prisca Japhes.
No comments: