SIMULIZI YA KWELI: BOB HAISA USO KWA USO NA SHAKILA.
“Nikiwa
na umri mdogo sana nilijikuta napenda kusikiliza muziki na hata nikiwa shuleni
mwalimu aliyeni vutia sana alikua wa michezo na muziki namkumbuka
Mwl. Julieti
aliyewahi kushika nafasi hiyo pale Mitindo shule ya msingi.
Siku za ijumaa tulitolewa mapema shuleni ili kujiandaa na swala ya
ijumaa, kiukweli nilikua nawahi nyumbani kwa lengo la kusikiliza muziki wa
mwambao kupitia RTD walikua wakipiga muziki huo muda wa saa saba mpaka saa
nane.
Mmoja kati ya watu walionivutia sana katika kipindi cha muziki wa
taarabu ni Bi Shakila ambae mara chache tu ndo kipindi kilimalizika bila wimbo
wake kwenda hewani, uimbaji wake ulitukuka sana nafsini mwangu hapo nilikua
mdogo kama miaka 12 hivi na tayari nilitamani kuimba muziki wa taarab ila
kwakua nilikua mdogo, nilitumia shauku hiyo kwa kushiriki uimbaji wa Qaswida
madrasa na kutumia vionjo vya Bi shakila katika kunakshi Qaswida jambo
lililonifanya niwe star kwenye madrasa.
Nilipomaliza shule ya msingi ilikua ndo mwisho wangu pia kushiriki
madrasa na Qaswida zangu zilitulia kwa muda mpaka nilipojikuta naibukia kwenye
muziki wa asili ya kisukuma baadae rap miduara na bongo flava ambapo umaarufu
wangu ulibebwa na miduara zaidi kutokana na single ya Nipe mgongo ambayo
ilipelekea niingia kwenye orodha ya waimbaji wa muziki wa pwani na kunipa
nafasi ya kukutana na wakali wengi wa muziki wa pwani wakongwe na wapya. Nakumbuka
siku ambayo sikuamini maskio yangu pale nilipopokea simu kutoka zanzibar sauti
nzito iliskika.
Haloo Asalaam alaikum, niliitikia kisha baada ya maelezo nilitambua
naongea na Yusuf Chuchu 'mungu amrehemu' na habari aliyonipa ndo ilinifanya
nisituke zaidi kwani ni mwaliko wa kupiga show ya pamoja na Bi Shakila Ooh
iliku siku nzuri sana kwani nilijikuta nakumbuka mengi sana na sikua na
pingamizi na safari ya zanzibar ikaanza kutoka dar mpaka Zanzibar.
Nilifika zanzibar na shauku yangu kubwa ilikua kumuona Bi Shakila
ambae tulikutana nae ndani ya Chuchu Fm hapa ilikua kati ya 2008 na 2009
kwakweli nilisikia sauti ya Bi shakila akiimba huku nikimuona live wakati
akifanyiwa mahojiano na hapo nilikumbuka mbali kwani licha ya umri wake kupea
bado sauti ilikua ileile sikusubiri tena bali alipomaliza zamu yake ya kuongea
tu nikamfata na kumnong'oneza ombi langu.
![]() |
Bob Haisa akiwa na Bi Shakila. |
Tafadhali mama naomba unifundishe kuimba, aliposkia neno lile
alitabasam kidogo akanambia tutaongea kisha tuliendelea na mahojiano na zamu
yangu ya kuhojiwa ilifuata baada ya joan, spider na wengine tuliokuanao pale
redioni, muda ulipotimia tulienda ukumbini na show ilikua moto sana, tulimaliza
na kubadilisha namba wote tuliokua tukitumbuiza pale ukumbini.
Siku iliyofuata ilikua jumapili jioni tulipokutana maeneo ya Forodhani
na baada ya kupata urojo mishikaki ya samaki, nyama na pweza kwa ndizi na
chips. Mbali na mapochopocho hayo jumapili, hiyo ndo siku tuliyokubaliana
kufanya kazi ya pamoja siku na saa ambayo hatukuipanga, tulitawanyika huku
nikifikiria kazi ya kushirikiana na Bi Shakila je iwe taarab mduara au reggae?
Sikupata jibu, miaka ikapita huku tukiwasiliana mara kadhaa mpaka
valentine day ya mwaka 2013 pale nilipoalikwa tena na ndugu yangu Richard
Luhende kwenda kutumbuiza morogoro sambamba na Bi Shakila tulipokutana
alinikumbusha Vp mpango wetu tatizo letu wasanii twapanga mengi halafu
hatutekelezi nilimuelewa alichomaanisha nikamjibu Mungu hajapanga siku
yetu.
Tukapiga show asubuhi tukaagana kwa kunywa chai pamoja mimi nikarudi
misungwi na Bi shakila akarudi dar”.
Itaendelea.....Na Bob Haisa
No comments: