LIVE STREAM ADS

Header Ads

DJ STIVE JUNIOR KUTOKA NCHINI KENYA ATUA JIJINI MWANZA KWA AJILI YA SHOW YA USIKU WA RAGGAE.

Ebwanaee hebu kamata huu mtonyo kutoka kwao One Drop Promotion ambae ni waandaaji wa Show Kubwa kabisa ya Reggae ambayo itadondoshwa kesho Octoba 03 ndani ya Villa Park Resort. Show hiyo imepewa jina la Reggae Bring Back Love itasimamiwa na
Dj mkali kutoka nchini Kenya Dj Steve Juniuor aka Roots Master ambae tayari amekwisha tua ndani ya Jiji la Mwanza-Rock City. Katika Picha (kushoto) ni Moses Manta ambae ni Mratibu wa Show hiyo huku (Kulia) akiwa ni Dj Steve wakati akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwanza.
Moses Manta (Kushoto) akisalimiana na Dj Stive Junior wakati akiwasili hii leo katika Uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya Show ya Reggae itakayopigwa kesho ndani ya Villa Park Resort kwa kiingilio cha shilingi Elfu Tano Tu.
Dj Stive Junior (Kushoto) akiwa na Moses Manta (Katikati) na George Binagi-GB Pazzo Blooer wa Mtanzaniamedia Blog (Kulia).
Safari ya Kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza ikawadia kwa ajili ya kuelekea Hotelini.
Dj Stive Junior akiingia katika katika gari kwa ajili ya kuelekea hotelini.
Dj Stive Junior (Mwenye Kofia) akiwa ndani ya gari kuelekea hotelini.
Baada ya Kufika Hotelini (Hotel Kingdom) ambapo Dj Stive (Katikati) na wenyeji wake wakafika ndani ya Villa Park Resort ambapo Show ya Reggae Bring Back Love itafanyikia Kesho. Mbali na Kufika hapa kwa ajili ya kujionea Mandhari ya Villa, pia eneo hili ni maalufu kwa upatikanaji wa Chakula safi hususani kwa wageni wanaoingia Jijini Mwanza hufika hapa kwa ajili ya kupata SAMAKI, Hivyo Dj Stive alifika hapa kwa ajili ya Kupata Msosi.
Kumbukumbu zikiendelea Mitaa ya Villa Park Resort hii leo.
Ile Dj Stive ameingia Villa, mara akakutana na jamaa akiwa na samaki akimtoa ziwani, zile mafoto si zikaanza sasa.
Ahsante kwa Kuitembelea Mtanzaniamedia Blog, Nikutakie Utazamaji na usomaji mwema wa Blog hii, Tukutane kesho ndani ya Villa Park Resort ili kupata Burudani ya Reggae kwa kiingilio cha shilingi Elfu Tano Tu.
SIKILIZA MAHOJIANO KATI YA GEORGE BINAGI @RADIO METRO & MTANZANIAMEDIA BLOG NA DJ STIVE JUNIOR KUTOKA NCHINI KENYA.

Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.