LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR NUSRA KUZICHAPA Llive HII LEO BUNGENI.

 Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akipiga kura leo kwenye ukumbi wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma kupitisha Sura na Ibara za Rasimu ya Katiba inayopendekezwa. 

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mh.Othman Masoud Othman ambae pia ni miongoni mwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, hii leo nursa kuingia katika historia nyingine baada ya vuta nikuvute baina yake na baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kutoka
Zanzibar kutokana na kupiga kura ya wazi na kukubaliana na naadhi ya ibara zilizomo katika rasimu ya Katiba inayopigiwa kura na wajumbe wa bunge hilo.

Timbwili hilo lilitokea muda mfupi baada ya bunge hilo kuahirishwa hii leo, ambapo duru za habari zinadokeza kwamba chanzo za mzozo huo kilitokana na baadhi ya wajumbe kutoka Zanzibar kuonekana kutofurahishwa na kitendo cha Mh.Othman kuzipigia kura ya HAPANA baadhi ya ibara zilizomo katika rasimu ya katiba inayopendekezwa na bunge hilo.

Baada ya Mabishano ya hapa na pale, Maafisa wa usalama ilibidi wamchukue Mh.Othman na kumuondoa katika eneo hilo kwa lengo la kupusha marumbano yaliyokuwa yakiendelea kati yake na baadhi ya wajumbe wenzie kutoka Tanzania Visiwani (Zanzibar) ambao habari zinaeleza kuwa hawakupendezwa na kitendo cha Mwanasheria Mkuu wa Zanzubar kupiga kura ya hapana. Tazama Matukio katika Picha.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akisindikizwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge Maalum leo mjini Dodoma na Askari Polisi. 
 Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (mwenye Kaunda suti ya kijivu) akisindikizwa kutoka nje ya viwanja vya Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma na Askari Polisi mara baada ya kushutumiwa na baadhi ya Wajumbe wa Zanzibar. 
 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mzee Kingunge Ngombale Mwiru pamoja Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara wakibadilishana mawazo kwenye viwanja vya bunge hilo mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mizengo Pinda (wa pili toka kulia) akibadilishana mawazo kwenye viwanja vya bunge hilo mjini Dodoma leo na wajumbe wenzie wa bunge Maalum la Katiba.  Wajumbe hao ni, Mhe. John Shibuda (kulia), Mhe. Mzee Kingunge Ngombale Mwiru (wa pili kushoto) na Mhe. Sophia Simba (kushoto).
Na Mwandishi Wetu.

No comments:

Powered by Blogger.