DK.TONNY KUTOKA RADIO METRO JIJINI MWANZA AOMBA KUUNGWA MKONO SIKU YA KESHO.
kuendelea kuwa na moyo wa kujitolea kutoa damu kadri iwezekanavyo kwa lengo la kuwa na hazina ya kutoka katika bank ya damu salama ili kuokoa maisha ya wahitaji wa damu pindi inapohitajika.
Dk.Tonny ambae ni Mtangazaji katika kipindi cha Pambazuko la Metro FM kinachoruka hewani Saa 12 hadi saa Tatu za asubuhi kuanzia jumatatu hadi ijumaa ndani ya Metro FM, aliyasema hayo hii leo Jijini Mwanza wakati akizungumza katika kipindi cha Metro Evening Drive kinachorushwa na Radio hiyo kila siku za jumatatu hadi ijumaa saa 10 alasiri hadi saa 12:30 za jioni.
Mpaka sasa pamoja na kukua kwa sayansi na tekenolojia, bado hakuna ugunduzi wowote ambao umebainika kuwa unaweza kusaidia watu kutengeneza damu kutokana na kuchanganya vitu mbalimbali, hivyo Watanzania lazima tuwe na moyo wa kujitolea kwa hiari kuchangia damu ili kuwasaidia watu mbalimbali hususani akina mama ambao hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua sanjari na wahitaji wengine kwa lengo la kuzuia vifo vinavyotokana na ukosefu wa damu".Alisema Dk.Tonny.
Katika kuunga Mkono juhudi hizo, Dk.Tonny amekuwa na desturi ya kuwahamasisha wananchi kuwa na moyo wa kujitolea kwa hiari kuchangia damu, ambapo kwa mara ya pili ndani ya mwaka huu zoezi la kuchangia damu litafanyika kesho katika Viwanja vya Shirika la Posta vilivyopo mkabala na Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza ambapo amewaomba wadau na wananchi mbalimbali kumuunga mkono hiyo kesho na kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuchangia damu kama walivyojitokeza katika awamu ya kwanza iliyofanyika miezi kadhaa iliyopita katika viwanja hivyo. Muda ni kuanzia saa Tatu kamili za asubuhi na Kuendelea.Kwa Mawasiliano zaidi piga simu nambari 0755 1969 06.
No comments: