LIVE STREAM ADS

Header Ads

TWIGA STARS KUMENYANA NA TIMU YA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MWANZA.

Wanahabari Mkoani Mwanza wakinasa Habari kuhusiana na Mechi inayotarajiwa kuchwa Jumapili ijayo katika ya Twiga Stars na Timu ya Watangazaji na Wanahabari Mkoani Mwanza katika dimba la CCM Kirumba.
Kutokana na Kanda ya Ziwa kuwa na Idadi kubwa ya akina Mama wanaosumbuliwa na Ugonjwa wa Kansa ya Shingo ya Kizazi, Taasisi ya Born To Help Foundatio Tanzania kwa Kushirikiana na
Kona ya Michezo ya Kwa Neema Radio ya Jijini Mwanza, wameandaa Mchezo wa Soka kwa lengo la kutafuta pesa zinakazosaidia katika kupambana na ugonjwa huo.

Mchezo huo ambao utapigwa Jijini Mwanza jumapili ijayo ya Octoba Tano katika Dimba la CCM Kirumba kuanzia majira ya saa 10 alasiri, utakuwa ni kati ya Timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” dhidi ya Mashujaa wa Kalamu na Sauti kwa maana ya Waandishi wa Habari na Watangazaji Mkoani Mwanza.

Akizungumza na wanahabari Mkoani Mwanza Mkurugenzi wa Born To Help Foundation ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha kona ya michezo katika kituo cha radio cha Kwa Neema Fm Erasto Juma alisema kuwa kutakuwa mbali na mechi hiyo baina ya watangazaji na wanahabari Mkoani Mwanza dhidi ya Twiga Stars pia kutakuwa na Mechi ya utangulizi kati ya Geita Venterans dhidi ya Matajiri wa Alimas, Mwadui Fc kutoka Mkoani Shinyanga, mechi ambayo itapigwa majira ya saa 8:00 za Mchana katika dimba hilo hilo la CCM Kirumba.

Aidha Juma alisema kuwa asilimia kumi ya mapato yatakayopatikana katika mchezo huo itapelekwa katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure kwa aajili ya kuwasaidia wanawake wanaosumbuliwa na saratani ya shingo ya kizazi huku akiongeza kuwa Kauli mbiu ya mchezo huo wa kijamii itakuwa ni "Tuungane na kupiga vita Kansa ya Shingo ya kizazi. Nani kama Mama”.

Kwa upande mwingine Juma alibainisha kuwa viingilio katika mechi hiyo vimepangwa kuwa ni sh.2,000 jukwaa la mzunguko na sh. 5,000 jukwaa kuu huku pia akiwataka wadau wadau, taasisi na makampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini mchezo huo kwa kuwasiliana naye kwa namba ya simu 0767 200 986.
Wanahabari Mkoani Mwanza wakinasa Habari kuhusiana na Mechi inayotarajiwa kuchwa Jumapili ijayo katika ya Twiga Stars na Timu ya Watangazaji na Wanahabari Mkoani Mwanza katika dimba la CCM Kirumba.
Na: Jacktan Msafiri

No comments:

Powered by Blogger.