LIVE STREAM ADS

Header Ads

UGONJWA SARATANI WATAJWA KUWA UGONJWA HATARI HAPA NCHINI.

Dr.Richard Mbwambo (Kushoto) ambae ni Meneja Kanda ya Ziwa kutoka Tume ya Kikiristo ya Huduma za Jamii nchini (CSSC) akiwa na Jim Cox (kulia) ambae ni Mkurugenzi wa Taasisi ya IMMA World Health katika Mkutano wa Uhamasishaji Viongozi wa Afya Mkoani Mwanza kuhusu kupambana na Ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi uliofanyika Gold Crest Hotel.
Ugojwa wa Saratani umetajwa kuwa miongoni mwa magonjwa hatari ambayo yamekuwa yakisababisha idadi kubwa ya vifo hapa nchini, huku idadi zaidi ya vifo hivyo ikielezwa kuwa husababishwa na Wananchi kuchelewa kufika Hospitalini kwa ajili ya Matibabu.

Hayo yalibainishwa hii leo Mkoani Mwanza na
Dr.William Kafura ambae ni Mratibu wa Saratani kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wakati akizungumza nje ya Mkutano wa Uhamasishaji Viongozi wa Afya Mkoani Mwanza kuhusu kupambana na Ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi.

Dr.Kafura alibainisha kwamba Ugonjwa wa Saratani umekuwa ukisababisha idadi kubwa ya vifo hapa nchini, ambapo Kansa ya Matiti na Kansa ya Saratani ya Shingo la Kizazi imekuwa ikifanya idadi hiyo kuongezeka zaidi hadi kufikia zaidi ya vifo 90 kwa siku hapa nchini.

Katika kupambana na hali hiyo alisema kuwa, Serikali kwa kushirikiana na Wadau wengine inafanya kila juhudi ili kuhakikisha kuwa huduma za matibabu zinapatikana katika Hospitali mbalimbali, tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo wagonjwa wa Saratani hutibiwa katika Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam.


Aidha alitoa rai kwa Wananchi kuwa na desturi ya kujitokeza kupima afya zao mara kwa mara kwa kuwa wagonjwa wengi wa Ugonjwa wa saratani hugundulika kuwa na ugonjwa huo huku wakiwa katika hali mbaya zaidi kutokana na kuchelewa kufika katika Vipimo.
Nae Dr.Safina Yuma ambae ni msimamizi wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia na Kukinga Saratani ya Mlango (shingo) ya kizazi alisema kuwa kuna mikakati mbalimbali imeanzishwa kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa lengo la kuhakikisha kuwa Wananchi wanapata uelewa wa kupambana na ugonjwa wa saratani.

Aliitaja Mikakati hiyo kuwa ni pamoja na Kutoa elimu kwa wananchi kwa kuwahamasisha kujichunguza mapema kwa kwenda katika vituo vya afya ili kama wakikutwa na maambukizi ya saratani waanze matibabu mapema kwa kuwa ugonjwa wa Saratani hutibika endapo kama mgonjwa atawahi matibabu.

Aidha Dr.Yuma alizitaja dalili za awali za ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi ambao umeonekana kuwa tishio kwa akina mama hapa nchini kuwa ni pamoja na Kuumwa na Tumbo chini ya kitovu kwa akina mama, kutokwa na majimaji yenye harufu ukeni, kutokwa na damu mfululizo ukeni hata katika siku ambazo si hata za hedhi pamoja na maumivu kuzunguka kiunoni.

Nae Dr.James Tumain Kengia ambae ni Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza alibainisha kuwa hali ya Saratani ya Kansa ya Kizazi ni kubwa Mkoani Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla, hivyo juhudi mbalimbali zinaendelea kufanyika ili kuhakikisha kuwa juhudi za kupambana na ugonjwa huo zinafanikiwa ambapo kwa Mkoa wa Mwanza uchunguzi wa dalili za awali unafanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure huku mikakati mingine ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba matibabu ya ugonjwa huo yanapatikana katika Hospital ya Rufaa ya Bugando.

Mkutano huo wa Uhamasishaji Viongozi wa Afya Mkoani Mwanza kuhusu kupambana na Ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi umefanyika kwa ushirikiano na Tume ya Kikiristo ya Huduma za Jamii nchini (CSSC), Taasisi ya IMA World Health pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii hapa nchini.

Dr.Safina Yuma (kulia) ambae ni msimamizi wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia na Kukinga Saratani ya Mlango (shingo) ya kizazi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akiwa katika Mahojiano na Paulina David (kulia) ambae ni Mwanahabari kutoa Radio Free Afrika (RFA).
Washiriki katika Mkutano.
Dr.William Kafura ambae ni Mratibu wa Kansa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (aliesimama kushoto) akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa Uhamasishaji Viongozi wa Afya Mkoani Mwanza kuhusu kupambana na Ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi.
Dr.William Kafura ambae ni Mratibu wa Kansa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akiwa katika mahojiano na wanahabari nje ya ukumbi wa mikutano.
Dr.William Kafura ambae ni Mratibu wa Kansa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akiwa katika mahojiano na wanahabari nje ya ukumbi wa mikutano.
Dr.James Tumain Kengia ambae ni Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza akiwa katika mahojiano na wanahabari nje ya ukumbi wa mikutano.
Dr.James Tumain Kengia ambae ni Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza akiwa katika mahojiano na wanahabari nje ya ukumbi wa mikutano.
Washiriki wa Mkutano wa Uhamasishaji Viongozi wa Afya Mkoani Mwanza kuhusu kupambana na Ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi wakiwa katika Mafunzo kwa Vitendo.
Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.