LIVE STREAM ADS

Header Ads

REGGAE BRING BACK LOVE NDANI YA ROCK CITY NA DJ STIVE JUNIOR KUTOKA NCHINI KENYA ILIKUWA BALAA.

Anafahamika kama Dj Stive Junior a.k.a Roots Master kutoka nchini Kenya akiwa kwa Mashine ya Villa Park Resort Jijini Mwanza usika wa kuamkia leo Octoba nne, ambapo jukumu lake lilikuwa ni Moja tu ambalo ni Kuangusha Burudani ya Mziki wa Reggae kwa Wapenzi wa Burudani Jijini Mwanza ambapo ilikuwa ni kwa Mtonyo wa Buku Tano tu Mlangoni.
Dj Stive Junior kwa Mashine akidondosha burudani ndani ya Villa Park Resort usiku wa kuamkia leo.
Dj.Stive Junior (Kushoto) akiwa na George Binagi (Kulia) ambae ni Blogger wa Mtanzaniamedia Blog.
Dj.Stive Junior (Kushoto) akiwa na George Binagi (Kulia) ambae ni Blogger wa Mtanzaniamedia Blog.
Dj.Stive Junior (Kushoto) akiwa na Moses Manta (Kulia) ambae ni Mratibu wa Show  ya Reggae Bring Back Love ambayo ilipigwa usiku wa kuamkia leo ndani ya Villa Park Resort Jijini Mwanza.
Dj.Stive Junior akianza amsha amsha zake baada ya kuingia ukumbini. Jamaa ni Mkali na kiukweli anaijua na kuithamini kazi yake ambayo sasa ni mwaka wake wa kumi akiwa katika kazi hiyo hususani akicheza mziki wa Reggae katika Level za Kimataifa.Mwenyewe anasema African Tour ndo imeanza hivyoooooooooooo.
Taswira ya eneo alilokuwa akifanyia makamuzi Dj Stive Junior.Hakika Heshima ziwaendee Villa Park Resort, Lenny Hotel ya Geita, Radio Metro Fm Jijini Mwanza, Kampuni ya Vinywaji Pepsi na Waandaaji wa Show hiyo iliyopewa jina la Reggae Bring Back Love ambao ni One Drop Promotions ambao walifanya mishe zote ili Dj Stive Junior atue nchini na kudondosha burudani kwa wakazi wa jiji la Mwanza lakini pia shukrani za pekee ziende kwa Media zote ndani ya Jiji la Mwanza za Support kubwa ziliyoionyesha katika Show hiyo.
One Love Mtanzaniamedia Blog-Kwa Pamoja, Tuijuze Jamii.

Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.