LIVE STREAM ADS

Header Ads

ANATAFUTWA BAADA YA KUPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA.

Hakimu Mstaafu Marco Odero Kiri (65) anaetafutwa na Familia yake baada ya kupotea katika Mazingira ya kutatanisha Jijini Mwanza.
Hakimu Mstaafu wa Mahakama ya Lamadi Mkoani Mara hajulikani alipo, baada ya kutoweka nyumbani kwake Jijini Mwanza katika Mazingira ya Kutatanisha.

Hakimu huyo
mstaafu anajulikana kwa jina la Marcco Odero Kiri anadaiwa kutoweka nyumbani kwake Mabatini Jijini Mwanza, takribani wiki mbili zilizopita.

Familia yake imeeleza kuwa alitoweka nyumbani kwake tangu Octoba 21 mwaka huu, ambapo imeelezwa kuwa mara ya mwisho alikuwa amevaa suruali nyeusi na shati la rangi ya kijivu lenye mikono mirefu huku miguuni akiwa amevaa viatu vyenye rangi nyeusi.

Tukio la kupotea kwake limeripotiwa katika Kituo cha polisi Kati Jijini Mwanza, hivyo yeyote atakaemwona anaombwa kutoa taarifa katika Kituo chochote cha Polisi kilicho karibu nae au kuwasiliana na familia yake kwa nambari za simu 0763 76  42 31 au 0784 01 36 36.
Mzee Marco Odero Kiri (65) anaetafuta na Familia yake baada ya kupotea katika Mazingira ya kutatanisha Jijini Mwanza.
IMETOLEWA NA WANAFAMILIA.

No comments:

Powered by Blogger.