LIVE STREAM ADS

Header Ads

DIALLO, MSUKUMA NA MAKONDA KATIKA ZIARA ZA HELKOPITA KATIKA MIKOA YA MWANZA NA GEITA.

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi ambao ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Antony Diallo (Wa pili kushoto) akifuatiwa na Katibu wa Hamasa wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Paul Makonda wakiwa katika Uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya kuanza ziara za Kichama kwa kutumia Helkopita katika Mkoa wa Mwanza. Ziara za Mkoani Mwanza pia zitamjumuisha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Joseph Msukuma.

Ziara hizo zimeanza


hii leo Novemba 17, 2014 katika Kata za Wilaya ya Sengerema, na kuendelea kesho Novemba 18,2014 katika Kata za Wilaya ya Magu na kutamatishwa Kesho kutwa Novemba 19 katika Kata za Wilaya ya Ilemela hii ikiwa ni katika Mkoa wa Mwanza. Ziara hizo zitaendelea katika Kata za Mkoa wa Geita kuanzia Alhamisi wiki hii ya Novemba 20,2014. Lengo la ziara hizo ni pamoja na Kuimalisha Chama kisiasa, Kuzungumzia mchakato wa Katiba Mpya, Kuimalisha Uadilifu ndani ya Chama sanjari na kuwasihi wananchi kujiandaa kushiriki kwa Utulivu na Amani katika chaguzi zijazo za Serikali za Mitaa.
Katibu wa Hamasa wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa Paul Makonda akiingia kwenye Helkopita tayari kwa ajili ya Kuanza ziara katika Kata za Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza.
Kikosi kazi cha Chama cha Mapinduzi CCM Kikiwa kiko tayari kwa ajili ya Ziara zake Mkoani Mwanza kwa Kutumia Chopa.
Endelea Kutembelea Mtanzaniamedia Blog ili Kwa Pamoja, Tuijuze Jamii.
Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.