LIVE STREAM ADS

Header Ads

YAMOTO BAND HAWAKUACHA DENI JIJINI MWANZA.

Wasanii wanaounda Kundi la Mziki hapa nchini Yamoto Band wakitumbuiza jana Novemba 16,2014 ndani ya Jembe ni Jembe Beach Jijini Mwanza ikiwa ni Show mahususi iliyoandaliwa Kifamilia zaidi na Kupewa jina la FAMILY DAY ambapo wale ambao hawakupata time ya kushuhudia burudani kutoka kwa wanamziki wa Kundi hilo Siku ya Ijumaa usiku basi jana waliweza kupata nafasi hiyo ambapo Show ilipigwa kifamilia zaidi.
Kundi la Mziki hapa nchini Yamoto Band ambalo lilikuwa Jijini Mwanza kuanzia Ijumaa Novemba 15 hadi Jana Novemba 16 mwaka huu likiwa na kazi ya
kuwaburudisha wakazi wa Jiji la Mwanza, limemaliza majukumu yake vyema na kuondoka bila kuacha deni kwa mashabiki wake.

Katika Show ya Kwanza iliyopigwa na Kundi hilo Ijumaa katika Fukwe za Jembe ni Jembe kundi hilo lilidondosha burudani kwa Mashabiki wake na hadi kufikia mwisho wa Show kila shabiki aliondoka eneo la tukio huku roho yake ikiwa imesuuzika vyema.

Katika show ya jana ambayo ilikuwa imeandaliwa mahususi kifamilia zaidi, pia kundi hilo lilidondosha burudani ya maana huku mashabiki waliohudhuria show hiyo wakionyesha dhahiri kuridhika na burudani kutoka katika kundi hilo.

Kwa Show zote mbili zilizodondohwa na Kundi hilo, ni dhahiri kwamba, Yamoto Band hawakuacha deni kwa Mashabiki wake ndani ya Jiji la Mwanza na Viunga vyake kwa kuwa kila alietoa pesa yake kwa ajili ya kwenda kupata burudani, basi aliipata kiasi cha kumfanya asuuzike roho yake.

Mbali na Yamototo Band, Pia kundi la vichekesho la Original Comedy jana liliweza kukonga nyoyo za mashabiki waliofika katika Fukwe hizo za Jembe ni Jembe, na hakika kila mmoja alicheka mpaka basi.Kiukweli Original Comedy ni Wachekeshaji na hata kama wewe ni Bingwa wa Kununa, mbele ya Kundi hili utacheka tu upende usipende.
Yamoto Band wakiwa kazini.
Shabiki akiwawatuza Vijana wa Yamoto Band.
"Mtu kula Milenda siyo ujinga ila Kupenda, Inzi kufa kwenye Kidonda siyo ujinga ila kupenda".
Mashabiki wakifurahia burudani kabambe kutoka kwao Yamoto Band katika Show iliyopigwa jana Jembe ni Jembe Beach.
Palikuwa hapatoshi, Mashabiki wa Yamoto Band walipata kitu roho inapenda.
Kundi la Original Comedy pia lilikuwepo ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu hata mmoja anaepaswa kununa akiingia Jembe ni Jembe Beach. Hapa Joti akikinukisha Jukwaani ambapo watu ilikuwa ni full Kucheeeeeekaaaaaaa.
Blogger Gsengo na Mwandishi wa Clouds Fm (Kushoto) akimsikiliza Joti (Kulia) kwa Umakini Mkubwa.
Majembe ya Original Comedy yakiwa Kazini.
Wasanii wa Kundi la vichekesho la Original Comedy wakicheza wimbo wa Yamoto Band-Niseme.
Hatimae Burudani ikawa imekamilika na hapa George Binagi-GB Pazzo MD wa Mtanzaniamedia Blog akakaa angle kupumzika baada ya pilika pilika za masaa takribani Matano ndani ya Jembe ni Jembe Beach.
Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.