WAANDISHI WA HABARI WAPEWA MAFUNZO YA USALAMA MTANDAONI.
Mtandao wa kutetea haki za binadamu Tanzania (Tanzania Human Rights Denders Coalition) (THRD) kwa kushirikiana na mtandao wa kutetea haki za binadamu wa Uganda wameaandaa kwa mafunzo ya usalama wa mtandaoni kwa waandishi wa habari wa Tanzania ili kuwapa ujuzi wa kuzuia taarifa zao kudukuliwa
Mafunzo hayo
yamewajumuisha wadau wa haki za habari ambao ni waandishi wa habari, bloggers na wafanyakazi kwenye sekta ya habari wapatao kumi na nane wakihudhuria mafunzo hato katika ukumbi wa Regency hotel Jijini Mwanza.
Akifungua mafunzo hayo mratibu wa THRD bwana Onesmo Ngurumo alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa waandishi wa habari wa kulinda taarifa zao hasa kwenye kuandika habari za uchunguzi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Ngurumo aliwataka washiriki wote kuzingatia mafunzo hayo kwa umakini kwa kuwa kwa sasa suala la kudukuliwa kwa taarifa limezidi kuongeza, lakini kwa kutumia mafunzo hayo waandishi wataweza kulinda taarifa zao kwa umakini kwa kutumia mbinu mbalimbali zitakazotumika.
Ngurumo alisema kuwa usalama wa mtandaoni kwa waandishi wa habari ni muhimu sana kwani kwa sasa watawala wengi hawapendi matumzi ya mitandao ya kijamii kutokana na kuhisi kuwa inawachafua na kuharibu mifumo yao ya kiutawala.
Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo toka Uganda bwana John Kaoneka alisema kuwa suala la udukuzi duniani limekuwa kubwa sana kiasi cha kulalamikiwa na Nchi mbalimbali, hivyo kuna kila sababu ya kila mtumiaji wa mtandao wakiwemo waandishi wa habari kufahamu kwa kina njia za kupambana na udukuzi ili kubabiliana na changamoto hiyo.
Naye mshiriki wa mafunzo hayo bwana Josephat Isango Ngimba alisema kuwa mafunzo hayo yatamsaidia kwa kiasi kikubwa cha kutumia mifumo mbalimbali ya kulinda taaarifa zake kwenye kompyuta yake.
Na:Edwin Soko-Dar es salaam
No comments: