LIVE STREAM ADS

Header Ads

MARUFUKU BODABODA KUJIHUSISHA NA MASUALA YA KISIASA NCHINI.

Makoye Kayanda ambae ni Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza.
Waendesha Pikipiki hapa nchini Maarufu kama Boda boda wametakiwa kutokujihusisha na masuala ya Kisiasa wakati wa Kazi ikiwa ni pamoja na kujumuishwa katika shughuli mbalimbali zikiwemo za kisiasa na baadhi ya wanasiasa wakati wa majukumu yao.

Kauli hiyo
imetolewa hii leo na Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoani Mwanza Makoye Kayanda wakati akizungumza na 99.4 Radio Metro na Mtanzaniamedia Blog kuhusiana na masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Umoja huo.

“Waendesha pikipiki wote Mkoa wa Mwanza pamoja na Tanzania kwa ujumla, ni ombi langu nawaomba sana tusijihusishe na siasa wakati wa kazi. Hatuzuii mtu kuwa na mapenzi na Chama chochote cha kisiasa lakini kwenye shughuli zetu tunapiga marufuku kwa sababu ukichanganya siasa na kazi si kazi tena…”.Alisema Kayanda huku akiongeza,

“Siasa na kazi ni vitu hatari, dini na kazi ni vitu hatari, ukanda na kazi ni vitu hatari, rangi na kazi ni vitu viwili tofauti. Fanye kazi ukimaliza nenda kwenye kazi nyingine unayotaka kuifanya…Taasisi zote zinazotaka kuzungumza na waendesha pikipiki ni vizuri zaidi zikapitia kwenye Umoja wa Waendesha pikipiki Mkoa, kwa maana ya kwamba taarifa ya waendesha pikipiki wanapokuwa wanazungumza na Taasisi fulani au mtu fulani au mwanasiasa fulani, ni vizuri Umoja utambue, lakini kama kila mtu atataka kuwafanya waendesha pikipiki anavyotaka tuko radhi kumshitaki…”.

SIKILIZA SAUTI YA MAKOYE KAYANDA HAPA CHINI.
Mafundi wa Pikipiki wakiwa katika Majukumu yao.
Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.