SIKU YA TAKWIMU DUNIANI, WANANCHI WATAKIWA KUTOA TAKWIMU SAHIHI PINDI ZINAPOHITAJIKA.
Goodluck Lyimo ambae ni Meneja wa Takwimu Mkoa wa Mwanza na Geita akiwa Ofisini kwake baada ya kutembelewa hii leo na 99.4 Radio Metro na Mtanzaniamedia Blog. |
Tanzania
hii leo inaungana na Mataifa mbalimbali duniani katika Kuadhimishwa Siku ya
Takwimu duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Novemba 18, ambapo kitaifa siku
hiyo inaaadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.
Akizungumza jana kuhusiana na Siku hii
Goodluck Lyimo ambae ni
Meneja wa Takwimu Mkoa wa Mwanza na Geita, amebainisha kuwa siku hiyo ilitengwa
mahususi kwa ajili ya kuhamasisha jamii na umma kwa pamoja kwa ajili ya
matumizi ya takwimu, lengo likiwa ni kusaidia katika Mipango ya Kimaendeleo.
Alisema katika Maadhimisho ya Kitaifa yanayofanyika Jijini Dar es
salaam mwaka huu, Machapicho mbalimbali yanayohusiana na Takwimu za Kitaifa
zilizokusanywa katika maeneo mbalimbali yatatolewa kwa wananchi.
“Maadhimisho haya kwa sasa yanashindwa kuandimishwa katika ngazi
ya Mikoa kutokana na ufinyu wa bajeti, japo malengo ya baadae ni kuhakikisha
maadhimisho haya yanaadhimishwa hadi katika ngazi ya Mikoa”.Alibainisha Lyimo.
Katika hatua nyingine Lyimo aliongeza kuwa, mbali na Sensa ya Watu
na Makazi ambayo hufanyika kila baada ya Miaka Kumi kwa ajili ya kutambua
takwimu za watu na Makazi, pia Ofisi ya Taifa ya Takwimu hufanya tafiti zake
mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa Takwimu za Mama na Mtoto lengo
likiwa ni kubaini idadi ya idadi ya Watu lengo likiwa ni kusaidia katika
shughuli za Maendeleo.
Hata hivyo Lyimo alibainisha kwamba bado kuna changamoto katika
upatikanaji wa Takwimu hapa nchini, kwa kuwa wanajamii wengi kuanzia ngazi ya
Kaya wamekuwa hawana desturi ya kutoa Twakimu zao sahihi.
Ametoa wito kwa wananchi kuwa tayari kutoa takwimu zao pindi
zinapohitajika kwa kuwa Umhimu wa Takwimu ni kwa ajili ya mipango ya
Kimaendeleo katika Taifa na si vinginevyo ambapo amewasihi baadhi ya wananchi
ambao wamekuwa na desturi ya kuficha takwimu zao kuacha desturi hiyo.
Radio Metro Fm pamoja na Mtanzaniamedia Blog baada ya kutembelea Ofisi ya Takwimu Mkoa wa Mwanza. |
No comments: