|
Balozi wa Kampeni ya mwanamke na uchumi Linah
Sanga (Mwenye Kinasa Sauti) akitoa burudani huku mkuu wa mkoa wa Tanga chiku galawa na mkurugenzi wa
Angels Moment wakifurahia pamoja naye ukumbini Nivera jijini Tanga |
Mkuu wa mkoa wa Tanga mheshimiwa Chiku Galawa amewataka
wanawake Mkoani humo kuwasaidia wanaume katika kazi mbalimbali za ujasiriamali
ili kuinua kipato cha kaya na familia zao.
Mheshimiwa Galawa alitoa rai hiyo
jana katika ukumbi wa Naivera
katika hotuba kwa wanawake na wajasiriamali wa mkoa wa Tanga wakati wa ufunguzi
wa semina za kampeni ya mwanamke na uchumi zilizoanza mjini hapa.
Alisema mkoa wa Tanga unao wanawake wachapa kazi na stadi wa
kujishughulisha isipokuwa wanakwamishwa na waume zao ambao wengi hubaki
vibarazani kwa kunywa kahawa na kucheza bao bila kujishughulisha.
“Tangu nimefika hapa Tanga imekuwa ikinishangaza sana kwa
jinsi wanaume zenu wanavyopenda kubaki nyumbani na kushindwa kufanya biashara
pamoja na ninyi wake zao,kila siku nashuhudia wanawake mkijishughulisha kwa
kazi mbalimbali za kuwaletea kipato,sasa mtapata mafunzo ya jinsi ya kufanya
biashara endelevu nawasihi nendeni na waume zenu kwenye biashara
zenu,shirikianeni katika biashara na matokeo yake yatakuwa mazuri” amesema
Alisisitiza kuwa ni aibu kwa vijana wa kiume kila siku kuomba
misaada maofisini wakati wangeweza kufanya kazi,jambo ambalo linachangiwa na
akina mama kutopenda kuwatuma kazi watoto wao wa kiume matokeo yake wanapokuwa
watu wazima wanakaa majumbani bila kujishughulisha kama ilivyo sasa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampeni ya Mwanamke na uchumi
Mahada Erick alisema kampeni ya mwanamke na uchumi inalenga kuibua hisia chanya
miongoni mwa wanawake juu ya maamuzi sahihi ya fursa za biashara na matumizi
sahihi ya rasilimali fedha na akiba.
Alisisitiza kuwa “Manunuzi ya vitu vingi visivyo vya lazima
yamefanya biashara za wanawake wengi kushindwa kukua na kushindwa kurejesha
mikopo kutoka taasisi mbalimbali walikokopa kwa kushindwa kuwa na nidhamu
katika matumizi na kukopa kwa kukosa malengo ya kibiashara, hivyo Kampeni ya
mwanamke na uchumi inaleta mawazo mbadala ya kujenga uwezo wa mwanamke wa mkoa
wa Tanga kwa kuangalia raslimali mpya kama ardhi na kujua hali za afya
itakuwa ni ukombozi kwa akina mama wengi”
Jumla ya wanawake 400 wanatarajiwa kupata elimu juu ya
kutambua fursa,afya bora na uchumi imara kwa mwanamke,usimamizi wa fedha na
uwekaji akiba pamoja na mwanamke na rasrimali ardhi,ambapo kwa mkoa wa
Tanga imewezeshwa na
NSSF,PPF,PSPF,GEPF,UTT,TBS,LEGAL NAIVERA,TANGA BEACH RESORT pamoja na SSRA.
|
Balozi wa Kampeni ya mwanamke na uchumi Linah
Sanga (Mwenye Kinasa Sauti) akitoa burudani huku mkuu wa mkoa wa Tanga chiku galawa na mkurugenzi wa
Angels Moment wakifurahia pamoja naye ukumbini Nivera jijini Tanga |
|
Balozi wa Kampeni ya mwanamke na uchumi Linah Sanga akitoa burudani huku
mkuu wa mkoa wa Tanga chiku galawa na mkurugenzi wa Angels Moment wakifurahia
pamoja naye ukumbini Nivera jijini Tanga. |
|
Burudani kutoka kwa Balozi wa Kampeni ya Wanawake na Uchumi Msanii Linah Sanga ikiendelea. |
|
Wanawake wajasiriamali mkoani Tanga wakifurahia
hotuba ya mkurugenzi wa Angels Moment Naima malima (Hayupo Pichani). |
|
MKUU WA MKOA WA TANGA MHESHIMIWA CHIKU GALAWA akitoa hotuba ya
ufunguzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi jijini Tanga leo,katika ukumbi wa
Naivera.
pix-6467 -Mkurugenzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi Mahada Erick
akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi mkoani
Tanga leo.
|
|
Mkurugenzi wa Kampuni ya Angels Moment Naima Malima akiwasilimia
wanawake wa Mkoa wa Tanga[hawapo pichani] katika ufunguzi wa Kampeni ya Mwanamke na Uchumi Mkoani humo uliofanyika siku ya jana.
|
|
Mkurugenzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi Mahada Erick akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi Mkoani Tanga uliofanyika jana. |
|
Balozi wa Kampeni ya mwanamke na uchumi Mwanamziki Linah Sanga. |
|
Wanawake wajasiriamali kutoka wilaya mbalimbali mkoani Tanga
wakifuatilia hotuba za mkuu wa mkoa wa Tanga[hayupo pichani] na ya mkurugenzi
wa kampeni ya mwanamke na uchumi. |
Na:Christian Gideon, Angels moment.
No comments: