LIVE STREAM ADS

Header Ads

JUBILEE YA MIAKA 50 YA CHUO CHA CBE, WANAFUNZI WA CHUO HICHO TAWI LA MWANZA WACHANGIA DAMU KWA HIARI.

Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Tawi la Mwanza hii leo wakimsikiliza kwa Makini Afisa Uhamasishaji Mpango wa Damu Salama Kanda ya Ziwa (Hayupo Pichani) kuhusiana na Umuhimu wa Uchangiaji wa damu salama kwa hiari. Hii ikiwa ni katika kuelekea katika Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha CBE yatakayofanyika January 25 Mwaka 2015.
Katika kuelekea Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE hapa nchini, Mwanafunzi wa Cho hicho Tawi la Mwanza wameamua kuungana kwa pamoja na kushiriki kwa hiari katika zoezi la uchangiaji wa damu.

Wakizungumza hii leo chuoni hapo na
Radio Metro & Mtanzaniamedia Blog, baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wameeleza kuwa wameguswa katika zoezi la uchangia wa damu kwa hiari kwa lengo la kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa damu hapa nchini.

Wamesema katika kipindi hiki ambacho wanaelekea katika Maadhimisho ya Miaka 5o tangu kuanzishwa kwa Chuo cha CBE kilichoanzishwa mwaka 1965, ni vyema wanafunzi hususani wa Sekondari na Vyuo wakawa na mwamko wa kuchangia damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wenye uhitaji wa damu.

Aidha wanafunzi hao wameshauri kuwa ni vyema elimu ya uhamasishaji juu ya kuchangia damu kwa hiari ikazidi kutolewa kwa vijana walioko mashuleni na vyuoni kwa kuwa elimu hiyo bado haijawafikia ipasavyo japo ambalo limekuwa likisababisha ugumu kwa vijana hao kujitokeza katika kushiriki zoezi la kuchangia damu kwa hiari.

Akizungumza juu ya hatua hiyo ya Chuo cha CBE Tawi la Mwanza kushiriki katika Zoezi la kuchangia damu, Amiri Shimbo ambae ni Mkufunzi Msaidizi idara ya Uhasibu Chuoni hapo amesema kuwa chuo hicho kimeamua kushiriki katika zoezi hilo kwa lengo la kuonyesha ushiriki wake katika jamii ikiwa ni katika kipindi cha kuelekea katika maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 yanayotarajiwa kufanyika Januari 25 mwakani.

Afisa Uhamasishaji Mpango wa damu salama Kanda ya Ziwa Bernadino Medaa amesema kuwa elimu zaidi juu ya uchangiaji wa damu kwa hiari inazidi kutolewa katika makundi mbalimbali katika jamii ambapo amebainisha kuwa kwa hivi sasa elimu hiyo imeanza kuwafikia watu wengi na hivyo kuonesha mafanikio makubwa katika zoezi la uchangiaji wa damu kwa hiari.
Wanafunzi wa Chuo cha Elimu  ya Biashara CBE Tawi la Mwanza wakimsikiliza Afisa Uhamasishaji Mpango wa Damu Salama Kanda ya Ziwa (Hayupo Pichani).
Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Tawi la Mwanza hii leo wakiwa katika Ukumbi wa Chuo hicho ambapo Afisa Uhamasishaji Mpango wa damu salama Kanda ya Ziwa (Hayupo Pichani) alikuwa akitoa elimu kwa wanafunzi hao juu ya Umhimu wa kuchangia damu kwa hiari kwa ajili ya kuokoa maisha kwa wahitaji wa damu.Baada ya elimu kutolewa kwa wanafunzi hawa pia zoezi la uchangiaji liliendelea chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho.mwaka 1965.
Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Tawi la Mwanza hii leo wakimsikiliza kwa Makini Afisa Uhamasishaji Mpango wa Damu Salama Kanda ya Ziwa (Hayupo Pichani) kuhusiana na Umuhimu wa Uchangiaji wa damu salama kwa hiari.
Mkurugenzi wa Chuo cha CBE Tawi la Mwanza Eustance Joel Mukayu (Kushoto) akiwa na Amiri Shimbo (kulia) ambae ni Mkufunzi Msaidizi idara ya Uhasibu Chuo cha CBE Tawi la Mwanza hii leo wakati wa utoaji wa elimu ya Uhamasishaji kwa wanafunzi wa Chuo hicho katika kushiriki zoezi la uchangiaji wa damu kwa hiari ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika kuadhimisha Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa CBE.
Bernadino Medaa ambae ni Afisa Uhamasishaji Mpango wa Damu Salama Kanda ya Ziwa akitoa elimu juu ya Umhimu wa Kuchangia damu hii leo kwa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Tawi la Mwanza.
Bernadino Medaa (Aliesimama Kushoto) ambae ni Afisa Uhamasishaji Mpango wa Damu Salama Kanda ya Ziwa akitoa elimu juu ya Umhimu wa Kuchangia damu hii leo kwa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Tawi la Mwanza.
Mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Tawi la Mwanza akitoa damu kwa hiari hii leo ikiwa ni katika kuelekea katika Maadhimisho ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho.
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Tawi la Mwanza wakitoa damu hii leo chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Maadhimisho ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mwaka 1965.
Zoezi la Uchangiaji wa damu kwa hiari likiendelea ambapo Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Tawi la Mwanza wamejitolea hii leo kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 ya Chuo hicho Maadhimisho ambayo yanatarajiwa kufanyika Januari 25 Mwakani (2015).
Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.