WATOTO WALIO CHINI YA UMRI WA MIAKA 18 KUPATIWA MATIBABU YA MACHO BURE MKOANI MWANZA.
![]() |
Mlemavu wa Macho akitumia kompyuta. |
Wito huo ulitolewa jana katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekou
Toure na
Mratibu wa Huduma ya Macho Mkoani Mwanza Dr.Elizabert Makamba katika
zoezi la utoaji wa huduma ya macho bure kwa watoto waliochini ya Umri wa Miaka
18.
“Matibabu ya macho yanaweza kutibiwa haraka ikiwa kama muathirika
atafikishwa mapema Hospitalini kwa ajili ya matibabu”. Alisema Dr.Makamba huku akiwasisitizia
wazazi na walezi kuwafikisha watoto wao walio
chini ya umri wa miaka 18 kwa ajili ya matibabu ya macho yaliyoanza
kutolewa bure jana Novemba 10 hadi Novemba
22 mwaka huu katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Kwa upande wake Meneja wa Huduma ya Mikoba kutoka CCBRT Oscar James
Tendeje alieleza kuwa Matibabu ya Mapema ya Macho husaidia kukuza shughuli za
Maendeleo hivyo ni vyema wakazi wa Kanda ya Ziwa wakajitokeza kwa
wingi katika huduma hiyo ya uchunguzi na utoaji
wa matibabu ya macho bure inayotewa kwa watoto walio chini ya umri wa Miaka 18.
Kwa Upande wao baadhi ya Wazazi na Walezi waliowapeleka Watoto wao
katika huduma hiyo kwa siku ya jana walitoa
shukrani kwa Madaktari wanaohusika katika
kufanikisha zoezi hilo ambapo nao waliwashauri wazazi na walezi wengine
kujitokeza kwa wingi na kuwapeleka watoto wao ili kupatiwa huduma hiyo.
Jana Novemba 10 nchi mbalimbali duniani kote ziliungana pamoja katika kuadhimisha
Siku ya Macho duniani ambapo katika Mkoa
wa Mwanza, Maadhimisho hayo yalienda sambamba na zoezi la upimaji na utoaji
wa matibabu ya bure kwa watoto walio
chini ya Umri wa Miaka 18 katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Seko
Toure, zoezi ambalo litafikia tamati Novemba 22 Mwaka huu.
Na:Jacktan Msafiri.
No comments: