WAENDESHA PIKIPIKI MKOANI MWANZA WAGOMEA ZOEZI LA UBADILISHAJI WA NAMBARI MPYA ZA PIKIPIKI.
Mwenyekiti wa Umoja huo
Makoye Kayanda alitoa kauli hiyo jana katika Mkutano Mkuu wa Umoja huo uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Elimu ya Mafunzo ya Ufundi VETA Mkoani Mwanza, Mkutano ambao ulienda sambamba na Uchaguzi Mkuu wa kuwachagua Viongozi wa Umoja huo.
Makoye alibainisha kuwa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza unapinga vikali zoezi la kubadili nambari za pikipiki kutoka zinazotumika hivi sasa kwenda katika nambari mpya, kutokana na zoezi hilo kuanza kutekelezwa huku waendesha pikipiki wakiwa hawajashirikishwa ipasavyo kwa lengo la kujua dhana nzima ya kubadili namba hizo.
"Huu ni mradi ambao tayari Serikali imeuanzisha kwa ajili ya baadhi ya watu ili kujipatia kipato.Najua Serikali imetoa muda wa miezi sita hadi kufikia mwakani mwezi wa tatu pikipiki zote ziwe zinatumia nambari mpya, lakini sisi Mkoa wa Mwanza hilo suala tutalipinga na tutakwenda mahakamani ili kupinga suala hilo".Alisema Makoye wakati akizungumza mapema kabla ya uchaguzi ambapo hata hivyo alitetea kiti chake kwa kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza.
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabara (RTO) Mkoa wa Mwanza, Koplo Frances Muganyizi ambae alikuwa Mgeni Rsmi akitokea kitengo cha Elimu Ofisi ya RTO Mkoa wa Mwanza aliahidi kufikisha masuala yote mhimu yaliyozungumzwa katika Mkutano huo wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya utekelezaji zaidi.
Katika Mkutano huo wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza, Makoye Kayanda alichaguliwa kwa awamu nyingine ya Miaka Mitatu kuwa Mwenyekiti kwa kupata kura 100 kati ya wajumbe 102 ambapo kura moja ilikuwa ya hapana huku moja nyingine ikiharibika ambapo Makamu Mwenyekiti aliechaguliwa ni Seif Kagoma ambae alipata kura 77.
Nafasi ya Katibu Mkuu ilienda kwa Abubakari Rubelwa ambae alitetea nafasi yake kwa kupata kura 98, huku Katibu Mkuu Msaidizi akiwa ni Dida Kinemo ambae alichaguliwa kwa kupata kura 99 kati ya Kura 102 za wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja huo.
Viongozi wa Vyama vya waendesha pikipiki walioalikwa kutoka Mikoa jirani katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza uliofanyika jana. |
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Umoja huo uliofanyika jana katika Chuo cha Elimu ya Mafunzo ya Ufundi VETA Mkoani Mwanza. Mkutano huo pia uliambatana na uchaguzi wa Viongozi wa Umoja huo. |
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Umoja huo uliofanyika jana katika Chuo cha Elimu ya Mafunzo ya Ufundi VETA Mkoani Mwanza. Mkutano huo pia uliambatana na uchaguzi wa Viongozi wa Umoja huo. |
Miongoni mwa wafadhiri wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza ambao ni Wauzaji wa Pikipiki aina ya FEKON wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Umoja huo jana. |
Maafisa Masoko kutoka Bank ya NMB wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza. |
Winniel Mahumbuga (Mwenye Kinasa Sauti) ambae ni Afisa Masoko kutoka Bank ya NMB Tawi la Kenyatta Jijini Mwanza akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza uliofanyika jana katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Chuo cha Elimu ya Mafunzo ya Ufundi VETA Mkoani Mwanza. |
Afisa Masoko kutoka Bank ya NMB Kanda ya Ziwa. |
Maxmillian Kailangana (Katikati) ambae ni Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoani Mwanza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.Kailanga alikuwa ni Mmoja wa wasimamiz wa Uchaguzi wa Kuwapata viongozi wa Umoja huo katika Kipindi ncha Miaka Mitatu ijayo. |
Msoma Shairi. |
Jackob Paul (Kushoto) ambae ni Mwenyekiti Umoja wa Waendesha Pikipiki kutoka Shinyanga akitoa salamu zake katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza. |
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Umoja huo uliofanyika jana katika Chuo cha Elimu ya Mafunzo ya Ufundi VETA Mkoani Mwanza. Mkutano huo pia uliambatana na uchaguzi wa Viongozi wa Umoja huo. |
Huu ndio Usafiri wetu na ndiyo uliotufikisha katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Chuo cha Elimu ya Mafunzo ya Ufundi VETA Mkoani Mwanza. |
No comments: