MABINGWA WA MASHINDANO YA MITUMBWI YA BALIMI EXRA LAGER 2014 MKOANI MWANZA WAPATIKANA.
Washindi wa Mashindano ya Mitumbwi Mkoa wa Mwanza Upande wa Wanaume wakipokea zawadi (Pesa taslimu Shilingi Laki Tisa) baada ya kuibuka Washindi wa Kwanza. |
Mashindano hayo yalifanyika katika Mwambao wa
Mwaloni Kirumba Jijini Mwanza ambapo kwa upande wa Wanaume Mtumbwi kutoka Sengerema uliokuwa ukiongozwa na Costantin Lusalage uliibuka bingwa wa Mashindano hayo na hivyo kujinyakulia kitita cha shilingi Laki Tisa.
Mwaloni Kirumba Jijini Mwanza ambapo kwa upande wa Wanaume Mtumbwi kutoka Sengerema uliokuwa ukiongozwa na Costantin Lusalage uliibuka bingwa wa Mashindano hayo na hivyo kujinyakulia kitita cha shilingi Laki Tisa.
Nafasi ya pili wanaume ilinyakuliwa na Mtumbwi kutoka Misungwi
uliokuwa ukiongozwa na Elisha Jacob na hivyo kujinyakulia Shilingi Laki Saba
huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mtumbwi kutoka Luchelele Jijini Mwanza
uliokuwa ukiongozwa na Emmanuel Masanyiwa na kujinyakulia shilingi Laki Tano na
hivyo kukamilisha nafasi tatu za Mitumbwi itakayoiwakilisha Mwanza katika
Fainali za Mashindano hayo ya Mitumwi Kanda ya Ziwa.
Kwa upande wa wanawake Mtumbwi
kutoka Misungwi uliokuwa ukiongozwa na Joyce Aron uliibuka nambari moja na
kujinyakulia zawadi ya Shilingi Laki Saba huku Mtumbwi uliokuwa ukiongozwa na
Tabu Daud kutoka pia Misungwi ukiibuka mshindi katika nafasi ya pili na kujinyakulia
shilingi Laki Sita na hivyo kukamilisha nafasi mbili kwa upande wa wanawake
katika fainali za Mashindano hayo Kanda ya Ziwa.
Katika mbio hizo za Mitumbwi mwaka huu, Ukerewe imepewa hadhi ya Kmkoa
hivyo mbio za kuwatafuta washindi kutoka Ukerewe zitafanyika jumamosi ijayo ya
Novemba 15 huko huko Ukerewe ambapo fainali za Mbio hizo za Mitumbwi Kanda ya
Ziwa zinatarajiwa kufanyika Desemba Sita Mwaka huu katika Mwambao wa Mwaloni
Jijini Mwanza.
Mabingwa wa Mashindano hayo upande wa wanaume walielezea kuwa
mashindano hayo yalikuwa na ushindani mkali lakini kutokana na kujituma katika
mazoezi wameweza kufanikiwa kuibuka mabingwa huku wakiongeza kuwa waandaji wa
mashindano hayo wanapaswa kuongeza zawadi kwa washindi kwa lengo la kuwasaidia
kujikimu kimaisha zaidi.
Washindi wa Kwanza (Mtumbwi kutoka Sengerema) upande wa wanaume katika Mashindano ya Mitumbwi Mkoani Mwanza wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi. |
Washindi wa Pili upande wa wanaume (Mtumbwi Kutokea Misungwi) wakipokea zawadi zao kiasi cha Shilingi Laki Saba. |
Washindi wa Pili upande wa wanaume (Mtumbwi Kutokea Misungwi) wakiwa katika picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi. |
Washindi wa Tatu upande wa Wanaume (Mtumbwi kutoka Luchelele Jijini Mwanza) wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi.Walijishindia Shilingi Laki Tano. |
Washindi wa Kwanza wa Mashindano ya Mitumbwi Mkoani Mwanza upande wa Wanawake (Mtumbwi kutoka Misungwi) wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi. Walijishindia shilingi Laki Saba taslim. |
Washindi wa Kwanza wa Mashindano ya Mitumbwi Mkoani Mwanza upande wa Wanawake (Mtumbwi kutoka Misungwi) wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi. Walijishindia shilingi Laki Saba taslim. |
Washindi wa Pili katika Mashindano ya Mitumbwi Mkoani Mwanza (Mtumbwi Kutoka Misungwi) wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi.Walijishindia shilingi Laki Sita. |
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ilemela (Katikati) tayari kwa kupuliza kipenga kwa ajili kuanza kwa mbio za Mitumbwi Mkoa wa Mwanza. |
"Tunashuhudia jama wanavyopiga Makasia". |
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ilemela (Kulia) ambae alikuwa Mgeni Rasmi katika Mashindano ya Mitumbwi yaliyofanyika jana Mkoani Mwanza. |
Edith Debwa (Kulia) ambae ni Meneja wa Bia ya Balidi Extra Lager akizungumza katika Mashindano ya Mitumbwi yaliyofanyika Jana Mkoani Mwanza katika Mwambao wa Mwaloni Kirumba. |
Malack Staki (Kulia) ambae ni Meneja Mauzo na Usambazaji Kanda ya Ziwa kutoka TBL akizungumza katika Mashindano ya Mitumbwi yaliyofanyika jana Mkoani Mwanza. |
Mbio za kuwatafuta mabingwa wa Kupiga Makasia katika Mashindano ya Mitumbwi Mkoani Mwanza zikiwa zimeng'oa nanga katika Mwambao wa Mwaloni Kirumba siku ya jana. |
Mtumbwi kutoka Sengerema ambao uliibuka nafasi ya Kwanza katika Mashindano ya Mitumbwi ngazi ya Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika jana katika Mwambao wa Mwaloni Kirumba Mkoani Mwanza ukiwasili. |
Mtumbwi kutoka Misungwi ambao ulishika nafasi pili katika Mashindano ya Mitumbwi Mkoani Mwanza ukiwasili katika fukwe za Mwaloni Kirumba Mkoani Mwanza. |
Burudani pia ilikuwa ni sehemu ya kunogesha Mashindano hayo ya Mitumbwi yaliyofanyika jana katika Mwambao wa Mwaloni Kirumba Mkoani Mwanza. |
Baadhi ya Wananzengo waliofika katika Mwambao wa Mwaloni ili kushuhudia Mashindano ya Mitumbwi mwaka huu 2014 katika ngazi ya Mkoa wa Mwanza. |
No comments: