 |
Wasimamizi wa Mradi wa Tibu Homa Unaoratibiwa katika Mikoa wa Kanda ya Ziwa wakizungumza na Waandishi wa Habari hii leo kuhusiana na Mradi huo (Hawapo Pichani). Kutoka Kushoto Mshauri wa Maboresho Mradi wa Tibu
Homa Kanda ya Ziwa Dr.Kristina Lugangira akifuatiwa na Victor Masbayi ambae ni Mkurugenzi Mradi wa Tibu Homa Kanda ya Ziwa (Katikati) na wa Kwanza Kulia ni Dr.Festus Kalokola ambae ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Mradi wa Tibu Homa Kanda ya Ziwa. |
Shirika la University Research Co.,LLC (URC) kwa kushirikiana na Wadau
wengine kupitia Mradi wa Tibu Homa, limelenga kuhakikisha kwamba linapunguza
maradhi na vifo vinavyotokana na magonjwa yanayosababisha homa katika Mikoa ya
Kanda ya Ziwa kwa watoto walio chini ya miaka mitano.
Katika hatua ya kwanza Shirika hilo limeanza
kufanya tafiti zake
katika Hospitali za Mikoa na Wilaya sanjari na Vituo mbalimbali vya Afya katika
Mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la Kubaini sababu zinazochangia vifo kwa
watoto pindi wanapokuwa wamefikishwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Hayo yamebainishwa hii leo Jijini Mwanza, Dr.Festus Kalokola ambae ni
Mkurugenzi wa Ufundi wa Mradi wa Tibu Homa Kanda ya Ziwa wakati akizungumza na
wanahabari kuhusiana na Mradi huo wa Tibu Homa.
Amesema kuwa baada ya kubaini sababu zinazosababisha vifo kwa watoto
wanaofikishwa hospitalini kwa ajili ya matibabu, itaweza kusaidia katika
kupambana katika kupunguza idadi ya vifo kwa watoto hususani wale ambao
wanafikishwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Kwa upande wake Mshauri wa UboresMradi wa Tibu Homa Kanda ya Ziwa
Dr.Kristina Lugangira ameeleza kuwa Mradi huo wa Tibu Homa umejikita katika
Malengo Makuu Matatu ambayo ni kuongeza upatikanaji na ufikiwaji wa huduma
mhimu za kinga na tiba kwa watoto chini ya miaka mitano, kuongeza mahusiano
katika jamii na vituo vya tiba ili kuboresha na kuongeza ufahamu na utumiaji wa
huduma za afya zitolewazo kwa watoto wenye homa chini ya miaka mitano huku
lengo la tatu likiwa ni kuhakikisha huduma muhimu za afya zilizoboreshwa
zinakuwa endelevu.
Awali katika Mkutano huo na Waandishi wa Habari Victor Masbayi ambae
ni Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Tibu Homa Kanda ya Ziwa, amebainisha kuwa kesho Alhamisi Novemba 12 hadi Ijumaa Novemba 13 kutakuwa na Mkutano ambao umelenga kuwakutanisha Maafisa na wauguzi wa Afya kutoka katika Wilaya na Mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na Wasimamizi wa Mradi wa Tibu Homa, kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali kuhusiana na Mradi huo ambapo Mkutano huo utafanyika katika Hotel ya Balaika Beach Resort iliyopo Ilemela Mkoani Mwanza.
Mshirika Mkuu wa Mradi wa Tibu Homa ni Shirika la University Research Co.,LLC (URC) kwa kushirikiana na Mshirika Mkuu Kitaifa ambae ni Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na wadau wengine ambao ni Shirika la Amref for Health Africa, Management Science for Health (MSH) chini ya Ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID) ambapo Mradi huo unatekelezwa katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita.
 |
Victor Masbayi ambae ni Mkurugenzi wa Mradi wa Tibu Homa Kanda ya Ziwa (Kushoto) akiwa na Dr.Festus Kalokola
ambae ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Mradi wa Tibu Homa Kanda ya Ziwa (Kulia). |
 |
Mshauri wa Uboreshaji katika Mradi wa Tibu Homa Kanda ya Ziwa Dr.Kristina Lugangira (kushoto) akiwa na Victor Masbayi ambae ni Mkurugenzi wa Mradi wa Tibu Homa Kanda ya Ziwa. |
 |
Victor Masbayi ambae
ni Mkurugenzi wa Mradi wa Tibu Homa Kanda ya Ziwa. |
 |
Mshauri wa Uboreshaji wa Mradi
wa Tibu Homa Kanda ya Ziwa Dr.Kristina Lugangira. |
 |
Wanahabari (Kushoto) Wakinasa Habari hii leo katika Ofisi za Shirika la Universty Research Co.,LLC (URC) zilizopo Isamilo Jijini Mwanza. Shirika hilo ni Mshirika Mkuu wa Mradi wa Tibu Homa unaoendeshwa katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.Kushoto ni Wasimamizi wa Mradi huo. |
Na:George Binagi.
No comments: