LIVE STREAM ADS

Header Ads

MATATA AMWAGA ZAWADI HADHARANI. AWATAKA WANANCHI KUONDOA TOFAUTI ZA KISIASA.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Henry Matata (Mwenye Kinasa sauti) akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kitangiri katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana Kitangiri Sokoni.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Henry Matata, ametoa rai kwa Wananchi kuweka pembeni tofauti zao za Kisiasa, na kuungana kwa pamoja katika kuendeleza juhudi za kimaendeleo.

Matata ambae
aliingia madarakani mwaka 2010 kama diwani wa Kata ya Kitangiri kupitia Chama cha Demokrasia na Maendelo Chadema, ameyasema hayo jana wakati akizungumza na Wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kitangiri Sokoni.

Akizungumza katika Mkutano huo kwa mwamvuli wa Chama cha Mapinduzi CCM kutokana na kutimuliwa ndani ya Chadema, Matata aliwasihi wananchi wa Kitangiri kuendelea kuwa na imani nae na kuweka tofauti za kivyama ambazo zilipelekea yeye kuondoka Chadema.

Amesema wakati anaingia madarakani Kata ya Kitangiri haikuwa katika hali nzuri kimaendeleo, lakini katika kipindi alichokaa madarakani ameweza kuleta maendeleo makubwa katika Nyanja mbalimbali ambazo ni pamoja na Elimu, Afya na Miundo mbinu.

“Mabarabara ya Kitangiri nimeyakuta katika hali mbaya sana na Serikali haina pesa, wakati mwingine mimi natoa pesa zangu kutengeneza barabara za wananchi wangu…lakini watu hawayaoni hayo…wakati mimi naanza kulikuwa hakuna shule, lakini sasa nendeni Jiwe kuu mkaone shule inavyofanya kazi...”.

Katika Mkutano huo pia Matata aliweza kuwatuza Wazee zawadi za Vitenge ikiwa ni sehemu ya kuonyesha mapenzi yao kwao kutokana na nmna ambavyo wamekuwa wakishirikiana nae vyema huku akiwaahidi vijana kuwa nao wajiandae na Supprise itakayofuata ambapo atawazadia ambapo hakuweka bayana amewaandalia zawadi gani.

SIKILIZA MASWALI NA MAJIBU HAPA CHINI.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Henry Matata (Mwenye Kinasa sauti) akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kitangiri katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana Kitangiri Sokoni.
Newton Mpoli ambae ni Mtendaji wa Kata ya Kitangiri (Mwenye kinasa sauti) akijibu baadhi ya Maswali yaliyokuwa yakiulizwa na Wananchi wa Kata hiyo mbele ya Mh.Henry Matata ambae ni Diwani wa Kitangiri (Mwenye sSuti).
Mmoja wa Wananchi wa Kitangiri (Kushoto) akimuuliza swali Henry Matata ambae ni Diwani wa Kata hiyo (Kulia).
Mmoja wa Wananchi wa Kitangiri (Mwenye Kinasa sauti) akimuuliza swali Henry Matata ambae ni Diwani wa Kata hiyo (Hayuko pichani).
Mmoja wa Wananchi wa Kitangiri (Mwenye Kinasa sauti) akimuuliza swali Henry Matata ambae ni Diwani wa Kata hiyo (Hayuko pichani).
Wanazengo wa Kata ya Kitangiri waliohudhuria Mkutano wa Diwani wao Mh.Henry Matata ambae pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela.
Mmoja wa Wananchi wa Kitangiri (Mwenye Kinasa sauti) akimuuliza swali Henry Matata ambae ni Diwani wa Kata hiyo (Hayuko pichani).
Baadhi ya Viongozi kutoka Kata ya Kitangiri Wilayani ilemela waliohudhuria Mkutano wa Hadhra wa Diwani wa Kata hiyo.Wa Kwanza kushoto ni Victorius Evodius ambae ni Mtendaji Mtaa wa Mediacal, Katikati ni Issa Salum ambae ni Mwenyekiti Mtaa wa Kitangiri A na wa Kwanza Kulia akiwa ni Kandra Mgejwa ambae ni Afisa Mtendaji Mtaa wa Kileleni.
Elizabeth Wangaluke ambae ni Mwenyekiti Mtaa wa Kitangiri B (Kushoto) akiwa na Newton Mpoli ambae ni Mtendaji Kata ya Kitangiri (Kulia).
Wananchi wa Kata ya Kitangiri waliohudhuria Mkutano wa Diwani wao Mh.Henry Matata ambae pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela.
Wananchi wa Kata ya Kitangiri waliohudhuria Mkutano wa Diwani wao Mh.Henry Matata ambae pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela.
Wanazengo wa Kata ya Kitangiri waliohudhuria Mkutano wa Diwani wao Mh.Henry Matata ambae pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela.
Wanazengo wa Kata ya Kitangiri waliohudhuria Mkutano wa Diwani wao Mh.Henry Matata ambae pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela.
Wanazengo wa Kata ya Kitangiri waliohudhuria Mkutano wa Diwani wao Mh.Henry Matata ambae pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza na Diwani wa Kata ya Kitangiri Henry Matata akionyesha Vitenge alivyowazawadia akina Mama na Wazee (Wake kwa waume) wa Kitangiri.
Zawadi za Vitenge zikiendelea kutolewa kwa Wananchi wa Kitangiri ambao ni Wamama na Wazee (Wake kwa waume).
Zawadi za Vitenge zikiendelea kutolewa kwa Wananchi wa Kitangiri ambao ni Wamama na Wazee (Wake kwa waume).
Zawadi za Vitenge zikiendelea kutolewa kwa Wananchi wa Kitangiri ambao ni Wamama na Wazee (Wake kwa waume).
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Henry Matata (Mwenye Kinasa sauti) akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kitangiri katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana Kitangiri Sokoni.
Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.