SERIKALI HAITAWAVUMILIA WATUMISHI WASIO WAADILIFU.
Serikali imewataka Maafisa Uvuvi wote hapa nchini kuhakikisha
kwamba wanatimiza wajibu wao wa kusimamia kikamilifi sheria za rasilimali za
uvuvi ambazo wamepewa dhamana ya kuzilinda.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt.Titus Kamani ametoa
kauli hiyo hii leo
Jijini Mwanza katika Mkutano wa siku moja wa Shirika la Hifadhi ya Jamii
(NSSF) na Wadau wa Sekta ya Uvuvi iliofanyika katika Hotel ya JB Belmont.
Kamani amesema kuwa Serikali haitawavumilia watumishi wasio
waadilifu ambao wataonekana kuenenda
kijunye katika kusimamia sheria za rasilimali za uvuvi hapa nchini ikiwa ni
pamoja na kujihusisha katika masuala ya uvuvi haramu.
Aidha amewaasa wananchi kuzithamni rasilimali za uvuvi ili
ziendelee kulinufaisha Taifa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadae kwa
kuwa ustaarabu ni pamoja na kutii sheria zilizopo bila shuruti.
Awali akizungumza katika Mkutano huo Crescentius Magori ambae ni
Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF, amesema kuwa katika Mkutano huo mpango wa
kuwawezesha wavuvi kujiunga na Mfuko wa NSSF umezinduliwa rasmi kwa Kanda ya
Ziwa na hivyo kuwasihi wavuvi kujiunga na Mfuko huo kwa ajili ya kunufaika na
mafao mbalimbali yanayotolewa na NSSF.
Washiriki wa Mkutano wa Shirika la Taifa la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Wadau wa Sekta ya Uvuvi Kanda ya Ziwa uliofanyika hii leo Jijini Mwanza katika Hotel ya JB Belmont. |

No comments: